Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Kusini, Hadija Mwema (katikati) akiwa na watumishi wa Mamlaka pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Usafirishaji Salama wa Kemikali yaliyofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Heritage Cottage – Msamala, mjini Songea, Ruvuma.
Washiriki wa Mafunzo ya Usafirishaji Salama wa Kemikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Kanda ya Kusini.
Meneja wa Mamlaka Ofisi ya Kanda ya Kusini, Hadija Mwema, akifungua mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali kwa madereva wanaosafirisha mizigo hatarishi yaliyofanyika katika ukumbi wa Heritage Cottage, Songea, Ruvuma Desemba 17 hadi 18, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima (wa tatu kushoto), wakiwa pamoja na wafanyakazi wa maabara ya uchunguzi wa udongo kwa ajili ya kutambua kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye udongo ya Assay Mine Lab. iliyopo wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Desemba 18, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima, wakikagua maabara ya uchunguzi wa udongo katika maabara ya uchunguzi wa udongo (Assay Mine Lab.) iliyopo wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Desemba 18, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia) na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima, wakikagua moja ya mitambo ya uchunguzi wa udongo kwa ajili ya kutambua kiwango cha dhahabu katika maabara ya udongo (Assay Mine Lab.) iliyopo wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Desemba 18, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa koti jeupe) akikagua maabara ya kupima udongo kwa ajili ya kutambua kiwango cha dhahabu kilichopo kwenye udongo iliyopo wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya, Desemba 18, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo (kulia) akiongea na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) mara baada ya kufika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa mazungumzo ya kikazi Desemba 17, 2024. Katikati ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Shenda, Kata ya Masumbwe Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mara baada ya kufika katika Kijiji hicho kwa ajili ya kufanya ukaguzi katika mialo ya wachimbaji wa dhahabu katika Kijiji cha Shenda Novemba 30, 2024.
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyevaa kofia nyeusi) akikagua moja ya mialo inayotumika kuchenjua dhahabu katika Kijiji cha Shenda, Kata ya Masumbwe ambapo wachimbaji hao wanatumia kemikali ya Zebaki katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.