Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea dawati la Mamlaka lililopo kwenye banda la Kliniki ya Biashara kwenye Maonesho ya Teknolojia ya Madini Septemba 22, 2023.
-
-
Mtumishi wa Mamlaka, Makusudi Jonathan (kushoto) wakitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya usajili wa kemikali kwa wananchi waliotembelea Banda la Mamlaka kwenye maonesho ya sita ya kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita kuanzia Septemba 20 hadi 30, 2023.
-
Wananchi waliotembelea banda la Mamlaka wakisani kitabu cha wageni baada ya kupata elimu kuhusu majukumu ya Mamlaka kwenye Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye uwanja wa EPZA Bombambili, mkoani Geita.
-
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka kwenye mafunzo ya wasimamizi wa kemikali.
-
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, cheti cha udhamini wa Kongamano la Pili la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika kuanzia Septemba 12 - 15, 2023, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) uliopo jijini Arusha. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama), akizungumza na watumishi wa Mamlaka, wadau wa kemikali na baadhi ya wageni (hawapo pichani), wakati akizindua Safari ya Utoaji Elimu kwa Umma kwa njia ya barabara kutoka Dar es Salaam mpaka Geita kuhusu kemikali aina ya “Sodium Cyanide” ambayo inatumika kuchenjua dhahabu kwenye migodi. Tukio la uzinduzi huo ulifanyika katika Ofisi ya Mamlaka jijini Dar es Salaam, Agosti 28, 2023.
-
Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP, Hassan Omary (katikati), akiwa pamoja na timu ya utoaji elimu kuhusu kemikali ya “Sodium Cyanide” na maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro baada ya kukamilisha mafunzo hayo.
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP, Pius Lutumo (aliyesimama), akizungumza wakati akifungua mafunzo kuhusu kemikali aina ya “Sodium Cyanide” kwa maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, yaliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Polisi Kibaha Agosti 28, 2023
-
Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga (kulia), akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kwenye Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi Agosti 24, 2023 katika viwanja vya Ruangwa. Kulia ni Meneja wa Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kusini Hadija Mwema
-
Meneja wa Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kusini, Hadija Mwema (kulia), akimsikiliza Kocha Msaidizi wa Timu ya Namungo, Shadrack Nsajigwa (kushoto) baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Lindi yanayofanyika katika uwanja vya Ruangwa uliopo wilayani Ruangwa.
-
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti Daniel Ndiyo (kulia), akizungumza na mdau anayejihusisha na masuala ya kemikali alipotembelea banda la Mamlaka katika Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji yanayofanyika Ruangwa mkoani Lindi.
-
Watumishi wa Mamlaka (waliovaa sare za blue) wakitoa elimu kwa Wananchi waliotembelea Banda la Mamlaka kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini, Mbeya.
-
Wananchi mbalimbali wakipata elimu kuhusu majukumu ya Mamlaka baada ya kutembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya kitaifa ya Nanenane yaliyofanyika jijini Mbeya.
-
Kamishna Jenerali, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya, Aretas Lyimo (kulia) akiongea na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima (kushoto) alipotembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mwakangale jijini Mbeya.
-
Madereva wanaosafirisha mizigo ya kemikali kutoka kampuni mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali yaliyoandaliwa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Mashariki na kufanyika Agosti 17-18, 2023, jijini Dar es Salaam.
-
Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (aliyesimama), akielezea majukumu ya Mamlaka yakiwemo utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ikiwemo kusajili wadau wote wanaojishughulisha na shughuli za kemikali kwa kutumia, kusafirisha, kusambaza na kuhifadhi katika Mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali kwa madereva yaliyofanyika kwenye ukumbi wa GCLA, jijini Dar es Salaam, Agosti 17, 2023.
-
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Takwimu, Omari Lugendo, akiwaongoza wakaguzi kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Wateja wa Kemikali ulioboreshwa (online portal II) katika Mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia uliofanyika jijini Dar es Salaam, Julai 1, 2023.
-
Wakaguzi na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia, wakimsikiliza Mgeni rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Lugwisha (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia.
-
Mwakilishi wa Wakaguzi, Esther Ishenda, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wakaguzi wengine wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia.
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Lugwisha, akiongea wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia Julai 1, 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wakati akifunga maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Arusha, Juni 25, 2023.
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akielezea kazi za uchunguzi wa kimaabara zinazofanywa na Mamlaka ikiwemo uchunguzi wa kimaabara wa vielelezo mbalimbali vya dawa za kulevya zinazowasilishwa na Mamlaka za udhibiti na vyombo vya ulinzi na usalama na utoaji wa ushahidi mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika wakati Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutembelea banda la Mamlaka kabla ya kufunga Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya, yaliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, Juni 25, 2023.Katikati ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyopewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutambua mchango wake kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), akiwa pamoja na watumishi wa Mamlaka ambao walishiriki maadhimisho hayo. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, Kagera Ng’weshemi, wa tatu kutoka kulia ni Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kaskazini, Eliamini Mkenga, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Sylvester Omary (wa pili kulia), Asha Ndwata (kulia), Glory Henji (kushoto) na Rukia Hassan (wa pili kushoto).
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima (wa tatu kushoto) wakiwa pamoja na Meneja wa Kiwanda TOL Tukuyu, Fredy Mwambuluma (wa tatu kulia) na watumishi wa Mamlaka walioambatana nao kutoka kulia Noela Ndekirwa, Anold Mapunda, Georgina Kilindo na Peter Chambia mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika kiwanda hicho uliofanyika Juni 7, 2023.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko na Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima, wakimsikiliza Mtaalam wa Maabara katika Kiwanda cha TOL Tukuyu, Igah Mwakyoma (aliyevaa fulana nyekundu) akieleza namna wanavyoweza kupima ubora wa gesi wanayozalisha kupitia maabara yao kabla ya kupakia kwenye magari kwa ajili ya kwenda kwa wateja wao kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (katikati), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Elias Mulima pamoja na Watumishi wa Mamlaka walioambatana nao wakimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha kuzalisha gesi ya Ukaa cha TOL Tukuyu, Fredy Mwambuluma (kulia) akieleza kuhusu namna shughuli za uchakataji wa gesi unavyofanyika katika kiwanda hicho wakati wa ukaguzi uliofanyika Juni 7, 2023.
-
Mgeni Rasmi, Profesa Tumaini Nagu (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka, Mkemia Mkuu wa Serikali na Wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi (Fizikia, Baiolojia na Kemia) ambao wamehitimu kidato cha nne na sita kwa mwaka 2021 na 2022 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Juni 1, 2023.
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (wa tatu kutoka kushoto), akimsikiliza Mtaalam wa Vinasaba kutoka Maabara ya Sayansi Jinai Baiolojia na Vinasaba, Leticia Waitara (kulia) baada ya kutembelea maabara ya Vinasaba kuona namna uchunguzi wa sampuli za vinasaba unavyofanyika katika ziara yake aliyofanya Juni 1, 2023.
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (katikati), akimsikiliza Kaimu Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Toksikolojia, Kagera Ng’weshemi (kulia) baada ya kutembelea maabara ya Toksikolojia kuona namna uchunguzi wa sumu unavyofanyika.
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (katikati), akiongea na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka wakiongozwa na Mwenyekiti, Prof. Esther Lugwisha (wa pili kushoto) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia) wakati Mganga Mkuu wa Serikali alipotembelea maabara za Mamlaka Jini 1, 2023, kuona namna taratibu za uchunguzi wa sampuli mbalimbali unavyofanyika
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (wa tatu kutoka kushoto), akiwapongeza walimu ambao masomo wanayofundisha katika shule walizotoka zimefanikiwa kutoa mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa kati ya wanafunzi bora katika masomo ya sayansi waliyopata zawadi.
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (wa tatu kutoka kushoto), akiwakabidhi vyeti wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi mwaka 2021 na 2022. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka, Prof. Esther Lugwisha, na kushoto kwake ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko
-
Wanafunzi wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi (Fizikia, Baiolojia na Kemia) ambao walihitimu kidato cha nne na sita kwa mwaka 2021 na 2022 iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 1, 2023.
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Esther Lugwisha, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (hayupo pichani) kuwasilisha hotuba yake ya ufunguzi wa hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam, Juni 1, 2023.
-
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu (aliyesimama), akizungumza na wanafunzi, walimu, wazazi pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi (Baiolojia, Fizikia na Kemia) waliohitimu kidato cha nne na sita kwa mwaka 2021 na 2022. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam, Juni 1, 2023. Profesa Nagu, ameipongeza Mamlaka kwa kubuni mbinu bora na mwafaka ya kuhamasisha vijana kupenda masomo ya sayansi.
-
Mwezeshaji wa Mafunzo, Murtaza Versi (kulia) akiwasilisha mada kuhusu “Organizational Culture” kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka na Sekretarieti yake yaliyofanyika Mei 18, 2023 katika Ofisi za Mamlaka, Makao Makuu, Dodoma.
-
Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Hussein Kakurwa (kulia) akiwasilisha mada kuhusu majukumu na wajibu wa Bodi wakati wa mafunzo kwa Wajumbe wa Bodi yaliyofanyika Mei 18, 2023, Dodoma
-
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka kushoto, Zubeda Salum, Dkt. Robert Malima, Dkt. Grace Kinunda na Dkt. Edda Vuhahula, wakiwa kwenye mafunzo kuhusu “organizational Culture” na mafunzo kuhusu usimamizi wa bajeti yaliyotolewa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Murtaza Versi katika ofisi za Mamlaka, Makao Makuu, Dodoma Mei 18, 2023.
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka, Profesa Esther Lugwisha (kushoto) na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kulia), wakifuatilia mafunzo kuhusu “organization Culture” yaliyotolewa na Murtaza Versi (hayupo pichani) kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka, Dodoma, Mei 18, 2023.
-
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka, Profesa Esther Lugwisha (kulia), Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa pili kulia), Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kusini, Hadija Mwema (wa tatu kulia) pamoja na Watumishi wa Mamlaka walioambatana nao wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote, Normandy Chan (kushoto) mara baada ya kufika katika kiwanda hicho kilichopo mkoani Mtwara kwa ajili ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Aprili 17, 2023. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Idara ya usimamizi na Udhibiti Ubora wa Kiwanda cha Dangote, Simon Kikota.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (wa tatu kushoto) akiongea na viongozi wa Kiwanda cha Dangote wakiongozwa na Meneja wa Machimbo ya Mawe, Mohamed Mndeme (kulia) wakati akifanya ukaguzi katika maeneo ya Kiwanda cha Dangote mkoani Mtwara Aprili 17, 2023.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto) akimpongeza Meneja wa Ofisi ya Kanda ya Kusini, Hadija Mwema (kulia) kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuiongoza Kanda hiyo wakati akitambulishwa rasmi kwa watumishi na kukabidhiwa Ofisi ya Kanda ya Kusini Aprili 17, 2023.
-
Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar, Dkt. Farid Mpatani (kushoto), akipata ufafanuzi kuhusu uchunguzi wa sampuli mbalimbali za mazingira unavyofanyika kwenye Maabara ya Mazingira kutoka kwa Mtaalam wa Maabara, Alois Ngonyani (kulia) wakati wa ziara ya kikazi aliyofanya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bara.
-
Katibu Msaidizi Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Dar es Salaam, Bi. Elizabeth Komba (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu Mkakati wa Mapambano dhidi ya Rushwa Mahala pa Kazi kwa watumishi wa Mamlaka na kuwasisitiza watumishi kuhakikisha wanakuwa waadilifu katika kusimamia shughuli za Serikali.