Ujumbe wa Mkemia Mkuu wa Serikali

Dr.Fidelice M.S.Mafumiko
CGC/CEO


 

 

Facebook   Twitter Instagram
Karibu GCLA

Karibu Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni maabara teule ya Serikali katika masuala ya uchunguzi wa kisayansi wa maabara. Ilianzishwa chini ya Shera ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Namba 8 ya mwaka 2016. Menejimenti ya Mamlaka inaongozwa na Mkemia Mkuu wa Serikali akisaidiwa na Wakurugenzi wa Idara, Meneja wa Kanda na Wakuu wa vitengo vinavyojitegemea katika utekelezaji wa sera na miongozo inayotolewa na Bodi Tendaji.

Historia ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inaanzia mwaka 1895 wakati wa kipindi cha Ukoloni wa Mjerumani ikiwa chini ya Wizara ya Afya kama kituo cha utafiti wa magonjwa ya Ukanda wa kitropiki kama malaria na kifua kikuu. Mwaka 1986 Maabara ya Mkemia Mkuu ikawa ni sehemu ya Idara zilizoko chini ya Wizara ya Afya, kabla ya hapo ilikuwa inaripoti kwa Mkurugenzi wa huduma za Hospitali katika Wizara ya Afya.

Mkemia Mkuu wa kwanza alikuwa Mjerumani, Bw. Gustav Giemsa, ambaye aligundua vidudu vinavyosababisha Malaria na vimelea vya Kifua kikuu, hii ilipelekea kitendanishi kinachotumika kugundua vijidudu  vya  ugonjwa wa malaria kwenye damu mpaka sasa hivi kufahamika kwa jina la “Giemsa Stain.”

Ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Makao Makuu, zipo pembeni ya Barabara ya Barack Obama, karibu na Taasisi ya Utafiti wa Saratani Ocean Road, Dar es Salaam.

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pia inasimamia utekelezaji wa Sheria tatu ambazo ni Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Nchini Namba 3 ya mwaka 2003, Sheria ya Vinasaba vya Binadamu (HDNA) namba 8, ya mwaka  2009 na Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Namba 8, ya mwaka 2016.

Dira Yetu

Kuwa maabara ya uchunguzi yenye hadhi duniani kwa ajili ya kushughulikia masuala ya afya,Ustawi wa jamii na mazingira.

Dhima yetu

Kutoa huduma bora za kimaabara na zenye gharama nafuu na udhibiti kwa serikali,taasisi,asasi na umma kwa ujumla kwa madhumuni ya kulinda afya ya binadamu na mazingira.

Habari Mpya
Jan 24, 2021
Dec 22, 2020
Dec 18, 2020
Oct 13, 2020