CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

 Askari wa kikosi cha Usalama barabarani na baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, wamenufaika na mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali hatarishi kutoka kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuwajengea uwezo zaidi katika kusimamia madereva wanaosafirisha kemikali na kuhakikisha wanazingatia sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2020.

Akifungua Mafunzo hayo Kamishna Mwandamizi wa Polisi Gregory Mushi kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amesema mafunzo hayo yatawasaidia askari wa kikosi cha usalama barabarani kuweza kuwadhibiti madereva wanaosafirisha kemikali hatarishi ambao watakuwa hawazingatii sheria na kanuni zilizopo na kuhatarisha maisha ya watu.

Kwa upande wake kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya Mashariki Danstan Mkapa amesema Mamlaka hiyo imechukua jukumu la kutoa mafunzo hayo ili kuweza kutoa fursa kwa Jeshi hilo kuweza kufahamu namna kemikali hatarishi zinavyoweza kusafirishwa, na madhara yanayoweza kujitokeza endapo usafirishaji wake hautasimamiwa kikamilifu.

Nae kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Pwani  Edson Mwakihaba  amesema ameishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo, kwani yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku hususani kwenye ajali zinazohusisha wa magari yanayosafirisha Kemikali hatarishi na kujiepusha na madhara yanayoweza kusababisha maafa mbalimbali.

Kamanda  wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Pwani Edson Mwakihaba akizungumza na maafisa wa kikosi hicho (hawapo pichani) wakati mafunzo kuhusu Usafirisaji salama wa Kemikali hatarishi ikiwa ni kuwajengea uwezo katika kusimamia madereva wanaosafirisha kemikali na kuhakikisha wanazingatia sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2020

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.