CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko amewataka wafanyabiashara wa kemikali za kuchenjulia dhahabu kuwajali wachimbaji wadogo kwa kuweka bei za kemikali ambazo wataweza kuzimudu ili wasiweze kufilisika.

Dkt. Doto Biteko ameyasema hayo jana wakati akipokea Maazimio ya mkutano wa wadau wa uingizaji, usambazaji na watumiaji wa kemikali ya kuchenjua madini ya dhahabu uliandaliwa na Tume ya Madini na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kufanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dodoma.

“Kuna sababu za ndani ambazo wafanyabiashara wameamua kuzitumia kutengeneza bei tofauti na bei halisia, kwa hiyo tumeamua kukutana hapa na ninaamini kwamba mtatusaidia kuja na maelekezo mahususi kwa watu wote waliopewa leseni ya kununua dawa za kuchenjua madini ili wauze kwa bei ya soko. Kwa bei hii inayouzwa hivi sasa hakuna mchenjuaji ambaye atapata faida kwasababu kama watanunua kemikali hiyo shilingi milioni 1.2 na bei ya dhahabu inashuka na kupanda maana yake wachimbaji watakufa” alisema Dkt. Biteko.

Amesema kufuatia kupanda kwa bei ya kemikali ya kuchenjulia dhahabu aina ya Sodium Cyanide kutoka shilingi 400,000 kwa dumu moja hadi shilingi 1.2 kumefanya wachimbaji wadogo kupata hasara.

“Asilimia 41.9 ya fedha zote za kigeni zinatokana na sekta ya Madini huku madini ya dhahabu yakichangia asilimia 90 ya kiasi hicho na pia, asilimia 50 ya mauzo ya bidhaa zote nje ya nchi yanatokana na madini huku asilimia 90 ya mauzo hayo yakitokea katika madini ya dhahabu” alisema.

Aidha, mkutano huo umeazimia kwamba, Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa bei elekezi ya kemikali ya kuchenjulia dhahabu aina ya Sodium Cyanide na kuifanyia mapitio kila baada ya miezi mitatu kwa lengo ya kulisimamia soko la bidhaa hiyo.

Aidha, mkutano umeazimia kwamba, wafanyabiashara wa kemikali hizo kuunda umoja wao kama ulivyoundwa wa wachimbaji wadogo ambao utakaowasaidia kujadili na kuwa na nguvu ya pamoja na Serikali iunde kikosi kazi cha kufuatilia suala la upatikanaji wa kemikali ya Sodium Cyanide nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi, Yahya Samamba, amesema, katika kipindi cha mwaka 2019 hadi Septemba 2022 jumla ya tani 39,564 za kemikali ya Sodium Cyanide ziliingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya kuchenjua madini ya dhahabu kwenye maeneo ya machimbo.

Copyright ©2023 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.