CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imezindua Safari ya Uelimishaji wa wadau na umma katika maeneo ambayo kemikali aina ya Sodium Cyanide inatunzwa na kupita wakati wa usafirishaji na kutumika kwa lengo la kuwapa uelewa kuhusu kemikali hiyo.

Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, amezindua safari hiyo Agosti 28, 2023 ambayo inatarajiwa kutoa elimu katika vituo (14) vilivyopo katika mikoa (8) ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na Geita ambapo uzinduzi umefanyika katika Ofisi za Mamlaka jijini Dar es Salaam.

“Kulingana na sifa na madhara mbalimbali ya kemikali zinazosimamiwa chini ya Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani, Sheria Na. 3 ya mwaka 2003 ya Usimamizi na Udhibiti na Kanuni zake zilizofanyiwa mapitio mwaka 2020, na umuhimu wake katika maendeleo ya kiuchumi. Sheria na Kanuni imeweka masharti mbalimbali ili kuwezesha kemikali hizo kuendelea kuingia nchini, kuhifadhiwa, kusafirishwa na kutumiwa bila kuleta madhara kwa afya na mazingira,” alisema Dkt. Mafumiko.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pius Lutumo, ameipongeza Mamlaka kwa kutoa elimu kwa Jeshi la Polisi Kada ya Ukaguzi mkoa wa Pwani kutoka Wilaya ya Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na Chalinze.

“Elimu hii imehusisha kemikali ambazo kimsingi ni hatari kwa binadamu hususani panapotokea ajali za kemikali barabarani. Hivyo, elimu hii imetutahadharisha sisi tunaokwenda kusimamia au kuokoa lakini pia wananchi kwa ujumla wanaofika maeneo ya ajali kuchukua tahadhari hasa wanapokutana na kemikali hatarishi,” alisema Lutumo.

Naye, Msimamizi Mkuu wa Shughuli za Operesheni, John Chipindula, amesema kuwa lengo la utoaji elimu kwa askari wa Jeshi la Polisi ni namna ya kutambua kemikali aina ya Sodium Cyanide, athari zake zinavyoweza kumuathiri binadamu kwa haraka na hatua gani za kuchukua pindi ajali za kemikali zinapotokea.

Copyright ©2023 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.