CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Zaidi ya tani elfu saba za kemikali aina ya Salfa zimeweza kuingizwa nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Agosti 2022 baada ya Serikali kuruhusu uingizwaji wa kemikali hiyo kwa njia ya kichele.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, wakati akifungua kikao cha wadau wa uingizaji na usafirishaji wa kemikali hatarishi aina ya Salfa, Ammonium Nitrate na Sodium Cyanide, Jijini Dar es Salaam.

“Hali ya udhibiti wa kemikali kwa sasa ni nzuri na unaridhisha kwa sababu utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Kemikali za Viwandani na Majumbani umefanyiwa mapitio na kuandaliwa kanuni zake za 2020 hivyo kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali za utekelezaji wa sheria zilizokuwepo.

Ili kwenda na wakati na kasi ya ushindani wa biashara, Serikali ya Awamu ya sita  kupitia Mamlaka imefanya mapitio ya Sheria ya Kemikali na Kanuni zake  na  hivyo kuruhusu uingizaji wa salfa kwa njia ya kichele jambo ambalo lilikuwa ni kilio cha wafanyabishara kwa muda mrefu”. Amesema Dkt. Mafumiko.

“Marekebisho ya sheria ya kemikali, imepelekea kuongezeka kwa mizigo ya kemikali kupitia Bandari ya Dar es Saam. Mfano kipindi cha Januari 2021 hadi Septemba, mwaka huu kemikali aina ya Ammonium nitrate tani 54,789 ziliingizwa nchini kwa matumizi ya ndani na tani 39,050 zilisafirishwa nchi za jirani. Aidha, tani 26,820 za Sodium cyanide zilingizwa nchini na kusafirishwa kwa ajili ya shughuli za uchenjuaji wa dhahabu migodini na hivyo kupelekea ongezeko la mapato na kuchangia ajira kwa watanzania”.

Dkt. Mafumiko alisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu zilizowekwa wakati wa uingizaji, upakuaji, upakiaji, ufungashaji na usafirishaji ili kulinda afya na mazingira ikiwa ni lengo kuu la Sheria, kwa vile kemikali nyingi hatarishi zinatabia ya kuwaka moto au kulipuka kama bomu mfano Ammonium Nitrate.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti, Daniel Ndiyo, amesema kuwa kikao hicho kimelenga kuweka mazingira wezeshi ya biashara ya kemikali ili kuendelea kukua na kuchangia katika pato la taifa bila kukiuka taratibu na hivyo kutimiza matakwa ya sheria ya kulinda afya za binadamu na mazingira

Copyright ©2023 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.