CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mawakala wa Forodha wa Mpaka wa Namanga wametakiwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani ili kuweza kutekeleza kazi zao kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini, Christopher Anyango, wakati wa zoezi la utoaji elimu kwa umma kwa Mawakala wa Forodha wa Mpaka wa Namanga katika Mkoa wa Arusha.

“Tunawambua nyie kama wadau muhimu kwetu katika utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Namba 3 ya Mwaka 2003, kwa sababu kazi kubwa ya wateja tuliowasajili mnazifanya nyie, kuanzia kuomba usajili mpaka kuomba vibali vya kemikali.

Wadau wengi wa kemikali tuliowasajili wanawatumia katika kuwezesha mizigo yao kuingia nchini na kutoka, hivyo mnapaswa kufahamu vizuri sheria ili mnapofanya kazi zenu za uwakala wa forodha mzingatia Sheria, kanuni na taratibu za uingizaji, uagizaji, utoaji na usaifirishaji wa mizigo ya kemikali nchini.

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kama msimamizi na mdhibiti wa kemikali, imeamua kutoa elimu kwenu juu ya majukumu yake ili muweze kutambua na kuzingatia mahitaji ya kisheria. Tunaamini kwa kufanya hivyo, mtafanya biashara kwa mafanikio ikiwa sambamba na kulinda afya na mazingira dhidi ya kemikali” alimaliza

Akizungumzia manufaa ya semina waliyopata, Mwenyekiti wa Mawakala wa Forodha katika Mpaka wa Namanga, Ismail Kilasi, alisema anaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa elimu waliyowapatia na anaamini itakuwa endelevu na kuzaa matunda katika kazi zao kwa kuboresha mahusiano na kuwezesha biashara.

“Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kweli ni moja ya taasisi za Serikali inayotoa huduma nzuri kwa hapa Namanga kwa mantiki ya uwezeshaji biashara, kwa sababu ukihitaji huduma unapata kwa wakati na kama kuna changamoto wanakueleza kwa wakati. Mfumo wa utoaji huduma kwa njia ya mtandao umesaidia kupunguza changamoto na tunaomba waendelee kwa kasi hiyo na idara nyingine za Serikali zifuate mfano wao ili kuboresha utendaji kazi.”

Copyright ©2021 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.