CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wahimizwa kuzingatia umahiri katika utendaji wa kila siku katika maabara zote ili kuongeza umahiri kwa watumishi, kuimarisha hadhi ya Maabara za Mamlaka pamoja na kuongeza wigo wa ithibati katika maabara.

Hayo, yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, wakati akifungua Kikao cha Menejimenti cha Mfumo wa Ubora wa Maabara kwa watumishi wa Kurugenzi ya Huduma za Sayansi Jinai kilichofanyika Novemba8,2022 katika ukumbi mdogo wa Bunge, jijini Dar es Salaam.

“Mamlaka imeandaa kikao hiki kwa lengo la kukidhi takwa la mfumo la kuonesha utekelezaji, ufanisi na uendelevu wa kiwango cha ISO/IEC 17025:2017, pia kupitia na kujadili utendaji wa mifumo ya ubora na malengo ya utendaji kazi,” amesema Dkt. Mafumiko.

Aidha, Dkt. Mafumiko, amewasihi watumishi wa Mamlaka kuendelea kuimarisha utendaji kazi wa Maabara uaozingatia viwango vya kimataifa ikiwa ni hatua muhimu ili matokeo ya maabara kuzidi kukubalika katika ngazi ya kimataifa.

“Ni jukumu la kila mtumishi kutambua nafasi yake katika kuuhishi mfumo na kuwajibika katika utekelezaji wa mfumo kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za maabara kupitia Ithibati,” ameongeza Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pia, Mkemia Mkuu wa Serikali, ameongeza kuwa, Mamlaka ipo katika utekelezaji wa Sera ya Umahiri (Competence Policy), kwa kupitia Kamati ya Mafunzo ambapo kila mtumishi atahitajika kupimwa umahiri wake katika utendaji wa kazi.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.