CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amewasisitiza wajumbe wa Kamati mpya ya Uadilifu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kufanya kazi kwa uaminifu na weledi ili kusaidia watumishi wa Mamlaka  kutekeleza majukumu yao kwa  uadilifu na uzalendo na kufikia viwango vinavyotarajiwa.

Dkt. Mafumiko ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya kamati hiyo kuhusu Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma yanayofanyika kwa siku mbili katika ofisi ya Makao Makuu ya Mamlaka jijini Dar es Salaam.

“Majukumu mengi ya Mamlaka hii ni nyeti hivyo Kamati ya Uadilifu ni muhimu kwa sababu ina nafasi kubwa katika kuhakikisha  watumishi wanazingatia uaminifu na uadilifu kwenye kazi zao za kila siku. Ni imani yangu kuwa kupitia kamati hii kila mtumishi atafanya kazi kwa uzalendo, utii, uadilifu na umahiri akijua kwamba anafanya kazi ambayo mwisho wa siku inapelekea maamuzi ya kisheria ambayo yanaweza kuleta athari ya moja kwa moja kwa mtu binafsi au kwa taifa,” alisisitiza Dkt. Mafumiko.

Pia alieleza kuwa Mamlaka imeandaa mafunzo ya kamati hiyo ili kuwapatia wajumbe misingi ya utekelezaji wa majukumu yao kimaarifa, kisheria, kiujuzi na kimtizamo ili kuendelea kujenga taswira nzuri ya taasisi kwa wadau na hata kwa Serikali ambayo ndiyo mdau mkuu.    

Aidha alitoa rai kwa wajumbe wa kamati hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kujali haki na uaminifu na kuhakikisha kila mtumishi anafanya kazi kwa ufanisi na uadilifu kwa maslahi ya taasisi na taifa kwa ujumla kwa sababu huo ndio msingi wa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka na suala hilo linapewa kipaumbele kikubwa na Mamlaka hiyo.

“Kamati hii ina jukumu kubwa la kuainisha viashiria vya uvunjifu wa maadili na kuwashauri watumishi kuchukua tahadhari dhidi ya vitendo vinayoweza kusababisha uvunjifu wa maadili lakini pia ina jukumu la kumshauri Mtendaji Mkuu na kumpa mapendekezo ya kukuza maadili katika taasisi hii,” alisema Dkt. Mafumiko.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Steven Agwanda alisema kuwa kamati hiyo ili ifanye kazi kwa ufanisi inatarajia ushirikiano kutoka kwa Menejimenti ya taasisi ambao ndio watoa maamuzi hivyo basi Menejimenti nayo ina nafasi kubwa katika kuhakikisha kamati hiyo inafanya kazi zake vizuri.

Kamati mpya ya Uadilifu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeundwa baada ya iliyokuwepo awali kumaliza muda wake na inatarajiwa kufanya kazi kwa muda wa miaka mitatu.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.