CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, imetoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia,Biolojia na Fizikia wa kidato cha nne wa mwaka 2019 na Kidato cha Sita mwaka wa mwaka 2020 tarehe 09 Julai 2021.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kutoa zawadi hizo, Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt.Fidelice Mafumiko, amesema nchi ya Tanzania ipo katika uchumi wa kati unaoongozwa na maendeleo ya viwanda, hatua ambayo inahitaji wataalamu wa kutosha katika kada za sayansi ambao watakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwenye viwanda vitakavyokuwa vinaongoza njia kuu ya Uchumi, hivyo ili kufika hili ni lazima nguvu ya kutosha itumike katika kuwatia moyo wanafunzi walioko mashuleni kupenda kusoma masomo ya Sayansi hasa Kemia, Biolojia na Fizikia.

“Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwa ni mnufaika wa wataalam wanaotoka na masomo haya na ndio maana imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi kwa kutoa zawadi na Vyeti kwa wanafunzi bora wa kike na wa kiume kwa kidato cha nne na sita  waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya Kemia,Biolojia na Fizikia kwa lengo la kuwahamasisha kupenda kusoma sayansi na kuisadia nchi katika maendeleo makubwa ya kisayansi na teknolojia ambayo yanahitaji taaluma ya wanasayansi.”.

Utaratibu huu umekuwa ukifanywa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa zaidi ya miaka kumi nne (14) ukiwa na lengo la kuongeza ari kwa wanafunzi hao na walimu wao kwa kujenga msingi imara ili kupata wataalam wataokwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia, huku mwaka huu idadi ya waliofanya vizuri ikiongezeka ikiwemo na ushindani ya shule za Serikali na binafsi.

“Ushindani kati ya shule na shule umeongezeka huku mwaka huu wanafunzi waliofanya vizuri kwa masomo ya Kemia, Baiolojia na Fizikia wanatoka kwenye jumla ya shule tisa kwa kidato cha nne na kumi na sita kwa kidato cha sita” alisema Dkt.Mafumiko.

Naye Elizabeth Mangu ambaye alipata zawadi akiwa kidato cha nne mwaka 2017 kwa somo la Baiolojia na mwaka 2020 akipata zawadi kwa somo la Kemia kidato cha Sita amesema siri kubwa ya mafanikio yake ni kumtanguliza Mungu na kufanya bidii muda wote akiwa shuleni huku akiwasihi wanafunzi walioko mashuleni kusoma kwa bidii hasa masomo ya sayansi na kuacha kuogopa kwa kuhisi masomo ya Sayansi ni magumu.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.