Mtumishi wa Mamlaka kutoka Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Protazi Lusabala (kushoto), akimuhudumia mdau wa kemikali aliyetembelea Mamlaka katika banda la huduma ya Kliniki ya Biashara ambayo ilihusisha Taasisi mbalimbali wezeshi katika masuala ya biashara katika Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wakati akifunga Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita, Oktoba 13, 2024.
Meneja Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Dastan Mkapa (katikati), akiwa na wadau wa Mamlaka pamoja na watumishi wa Ofisi ya Kanda ya Mashariki katika hafla fupi ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika jengo la Ushirika jijini Dar es salaam, Oktoba 11, 2024.
Msimamizi wa dawati la Utawala na Fedha, Sophia Nuru (kushoto) akiwalisha keki wateja waliofika katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyofanyika jengo la ushirika jijini Dar es salaam, Oktoba 11, 2024.
Mmoja wa Wadau wa Mamlaka kutoka kampuni ya Keds Tanzania Company Ltd. Jenipher Shuma (katikati) akikata keki katika hafla fupi ya kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Meneja Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa, akiongea kwenye hafla fupi ya kuhitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, iliyofanyika katika jengo la Ushirika jijini Dar es salaam, Oktoba 11, 2024.
Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti, Daniel Ndiyo (katikati), akiwa na Kaimu Meneja wa Maabara ya Chakula na Dawa, Everlight Matinga (kulia) wakifurahia Tuzo ya Mshindi wa pili iliyopata GCLA kwa Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Oktoba 12, 2024.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wakifurahia Tuzo ya Mshindi wa Pili kwa Taasisi wezeshi za Serikali katika sekta ya madini kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Oktoba 12, 2024.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (katikati), na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella (mwenye shati jekundu) pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka, Daniel Ndiyo (aliyeshika tuzo) wakiwa pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wanaoshiriki maonesho baada ya Mamlaka kuibuka washindi wa pili kwa Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini, kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Oktoba 12, 2024.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (kushoto), akimkabidhi Tuzo Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Mamlaka, Daniel Ndiyo (kulia) baada ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kuibuka mshindi wa pili katika kipengele cha Taasisi Wezeshi za Serikali katika Sekta ya Madini kwenye Maonesho ya 7 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Oktoba 12, 2024.