CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko ameshuhudia utiaji saini wa hati ya Makubaliano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na Dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Upande wa Serikali, makubaliano hayo yamefanyika baina ya Mamlaka ya kudhibiti ya kupambana na Dawa za kulevya chini ya Kamishna Jenerali, Gerald Kusaya na wawakilishi wa Sekta binafsi huku Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ikishuhudia utiaji saini wa makubaliano hayo kwa kuwa ndio wanaopaswa kisheria kusimamia uingizwaji wa Kemikali nchini.

Mkemia Mkuu wa Serikali,Dkt.Fidelice Mafumiko amesema lengo la serikali kupitia sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali, sheria Na.3 ya mwaka 2003 ni kuweka utaratibu na  kuwezesha matumizi salama ya kemikali katika nyanja mbalimbali hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha hili linafuatwa.

Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya amesema kuwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi ni muhimu sana katika kukabiliana na changamoto ya uchepushaji wa kemikali bashirifu ukizingatia kati ya mwaka 2015 na 2017 nchi yetu ilikuwa na changamoto ya usafirishaji haramu wa kemikali bashirifu na dawa zenye asili ya kulevya na nchi yetu ikifanywa kama kituo cha kusafirishia bidhaa hizo.

Hafla hiyo fupi imefanyika katika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam tarehe 31 Agosti, 2021.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.