CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

MKEMIA MKUU ASISITIZA USIMAMIZI WA SAMPULI ZA JINAI KWA JESHI LA POLISI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka askari wa jeshi la polisi na wapelelezi kuzingatia umakini katika uchukuaji, utunzaji na usafirishaji wa sampuli au vielelezo vya jinai ambavyo uwasilishwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi wa kimaabara kwa ajili ya mashauri ya jinai yaliyopo katika vyombo vya sheria.

Mkemia Mkuu wa Serikali amesema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya uchukuaji, usafirishaji na utunzaji wa sampuli na vielelezo yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa askari wa jeshi la polisi katika Chuo cha Polisi Zanzibar.

“Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni mdau mkubwa wa Jeshi la Polisi katika kusaidia kukamilika kwa upelelezi wa makosa mbalimbali ya jinai yanayohusisha uchunguzi wa kimaabara wa sampuli au vielelezo. tumekuwa tukipokea sampuli na vielelezo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara baadhi vikiwa na changamoto. Changamoto hizo ni pamoja na sampuli au vielelezo kutokidhi vigezo vya uchunguzi wa kimaabara, mapungufu katika nyaraka zinazowasilishwa, utunzaji wa sampuli na vielelezo katika mazingira yasiyofaa pamoja na kutumia vifungashio visivyofaa vinavyosababisha kuharibika kwa sampuli. Changamoto hizo ni kama kutumia vifungashio visivyofaa na utumiaji wa plastiki kuhifadhia sampuli za vinasaba ambazo hazijakauka” alisema.

Dkt. Mafumiko alisema Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa mafunzo hayo kwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kukumbushana na kutatua changamoto za sampuli zinazowasilishwa kwa ajli ya uchunguzi wa kimaabara kuwa na ubora utakaowezesha uchunguzi kufanyika kwa haraka na kutoa majibu kwa wakati.

“Lengo la mafunzo haya ni kukumbushana namna bora ya uchukuaji wa sampuli kutoka kwenye eneo la tukio au kutoka kwa muathirika, ufungashaji, uhifadhi, utunzaji, uandaaji wa nyaraka pamoja na uzingatiaji wa mlolongo mzima wa  uwasilishaji wa sampuli hadi kufika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Matarajio yangu, mtakuwa mabalozi wazuri wa kueneza elimu hii kwa wenzenu ambao hawakupata nafasi ya kushiriki mafunzo haya. Ni matumaini yangu pia kuwa mafunzo haya yatakuwa endelevu kwa miaka inayofuata” alimaliza.

Aidha, Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Augustino Senga, akiongea, alisema wanafarijika kwa elimu waliyopata kwa sababu imewafanya kuwa wapya na kutawasaidia kutoharibu kesi kutokana na uharibifu wa sampuli au vielelezo hasa kwa kundi hilo la askari ambao ni uwakilishi wa nchi nzima.

“Tunashukuru kwa mafunzo haya maana kwetu kama Jeshi la Polisi ni neema, hapa kuna uwakilishi wa Tanzania nzima. Mlichotufundisha kitasambaa nchi nzima, tuendelee kushirikiana kwenye eneo la mafunzo kwa sababu mna kitu cha kutuelimisha nasi tunacho kitu hivyo, tuishirikiana tutaweza kufanikisha mambo mengi” alimaliza.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.