CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Waajiriwa wapya wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wametakiwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma, kutunza siri za Mamlaka, kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja kutoa taarifa kuhusu vihatarishi watakavyobaini wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, Dar es Salaam Januari 2, 2023 wakati akifungua mafunzo ya awali kwa wajiriwa wapya na watumishi waliohamia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), ikiwa lengo ni kuwawezesha kufahamu majukumu na utamaduni wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuwajengea hali itakayowafanya wajiamini na waweze kutekeleza majukumu watakayokabidhiwa kwa ufanisi.

 “Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni miongoni mwa taasisi nyeti za Umma ambayo inahitaji watumishi si wenye weledi pekee bali pia wenye uadilifu wa hali ya juu. Uadilifu unasisitizwa kwa kuwa, kukosekana kwa uadilifu katika Mamlaka kutapelekea madhara makubwa kwa Serikali na Umma kwa ujumla kutokana na asili ya majukumu yetu,” amesema Dkt. Mafumiko.

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa, watumishi hao watunze siri za Mamlaka ili kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutoa taarifa kuhusu vihatarishi mbalimbali utakavyobaini wakati wa kutekeleza majukumu yao, kujisimamia mwenyewe kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma, kufanya maamuzi kwa kuzingatia utaalam walionao na taratibu zilizopo za Serikali.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi za Huduma za Taasisi, Matrida Lugenge, amewaasa waajiriwa hao kuhakikisha wanatumikia umma kwa weledi, bidii, kujitoa na kuweka mbele maslahi ya taasisi na taifa kwa ujumla.

Naamini, baada ya mafunzo haya mtaweza kutumia vizuri muda wenu wa kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi lakini kuhakikisha mnasimamia kwa umakini rasilimali za umma ziweze kutumika kama ilivyokusudiwa,” aliongeza Matrida.

Copyright ©2023 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.