CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka Wajasiriamali wanaotumia kemikali katika uzalishaji wa bidhaa kuzingatia matumizi salama ya kemikali hizo.

Mkemia Mkuu wa Serikali amesema hayo leo wakati akifunga mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati wanaotumia kemikali yaliyoandaliwa na Ofisi ya Kanda ya Mashariki na kufanyika Ukumbi wa NSSF uliopo Ilala, Dar es Salaam.

“Kemikali ni hatari zisipotumiwa kwa uangalifu kwa sababu inaweza kutumika kama silaha, kwa sababu mtu akimwagiwa usoni inaweza kusababisha upofu. Matumizi yakiwa mabaya yanaweza kuleta madhara kwa nchi kama ilivyotokea nchini Lebanon kwa kemikali kulipuka na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Namba 3 ya Mwaka 2003, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepatiwa jukumu la kutoa elimu na mafunzo kuhusu Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa wadau wanaojishugulisha na kemikali kama Wajasiriamali kwa lengo la kuwa na weledi katika matumizi ya kemikali na uelewa wa kutosha kuhusu kemikali na madhara yake ili kuweza kuzitumia kwa faida ili kujipatia kipato na wakati huo huo kulinda afya za binadamu na mazingira.

Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yamebadilisha mitazamo yenu juu ya matumizi ya kemikali na itakuwa chachu kwenu kama Wajasiriamali kuzingatia masharti ya matumizi salama ya kemikali,” alimaliza.

Akiongea kwa niaba ya Wajasiriamali waliohudhuria mafunzo hayo, Agnes Kuratha, aliishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Kanda ya Mashariki kwa kuandaa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo na maarifa zaidi Wajasiriamali wanaotumia kemikali katika shughuli zao za kibiashara.

“Tunatanguliza shukrani zetu za dhati na tunawapongeza kwa kuandaa mafunzo haya ya matumizi salama ya kemikali, mmetusapoti na mmetupa mwanga mkubwa kuhusu matumizi salama ya kemikali, ambapo yatatusaidia kuweza kupiga hatua katika shughuli zetu za kijasiriamali lakini pia kulinda afya zetu na mazingira.”

Copyright ©2021 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.