CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

WANACHAMA WA TAMAVITA WAHIMIZWA KUZINGATIA MAFUNZO YA MATUMIZI YA KEMIKALI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka wanachama wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA), kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), ili kuweza kupata elimu ya msingi ya kufahamu huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali hasa kwenye elimu ya matumizi salama ya kemikali.

Dkt. Mafumiko ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wanachama wa TAMAVITA, yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (JNICC), Dar es Salaam, Septemba 2, 2022.

“Ninyi ni sehemu muhimu katika jamii ya Watanzania, hivyo, Mamlaka inatoa mchango wa kuwapa elimu ya msingi ya kemikali kwenu ambao mnajihusisha na shughuli za kemikali. Tunaamini kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunatimiza wajibu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa huduma kwa jamii hususani kwa makundi maalum ambao mnachangamoto ya usikivu ambao kuna muda inakuwa vigumu kwenu kupata taarifa muhimu kupitia baadhi ya vyombo vya habari. Mafunzo haya yatawawezesha kuwa na uelewa wa pamoja na kuweza kutumia kemikali bila kuwaleta madhara,” alisema Dkt. Mafumiko.

Aidha, Mkemia Mkuu ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo kuwa mabalozi wazuri wa kueneza elimu kwa jamii inayohusu majukumu ya Mamlaka kwa wanachama wenzao, ndugu, jamaa na marafiki.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania (TAMAVITA), Kelvin Nyema, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutoa mafunzo ya matumizi salama ya kemikali ambayo ni muhimu sana kwa viziwi na Zaidi yamewasaidia kufahamu athari za kemikali na sumu. Ameomba Mkemia Mkuu wa Serikali kuendelea kushirikiana ili kuwafikia wanachama wengi zaidi wa TAMAVITA wa mikoa mingine na kuwapatia elimu ya matumizi ya kemikali.                                                      

 

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.