CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Madaktari wanafunzi wa mwaka wa tano katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba cha Kikristo Kilimanjaro wametakiwa kuzingatia misingi na taratibu za uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara zinazopelekwa kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi Jinai na Vinasaba .

Akiongea wakati wa mafunzo ya uchukuaji na utunzaji wa  sampuli za uchunguzi wa Vinasaba vya Binadamu na Toksikolojia yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa wanafunzi hao, Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias, amesema madaktari ni moja ya wadau muhimu katika uchunguzi wa kimaabara unavyofanywa na Mamlaka katika masuala ya jinai na tiba hivyo mafunzo hayo ni kama sehemu ya kukumbushana kwa madaktari hao wanaotarajia kwenda kufanya kazi maeneo mbalimbali nchini kuhusiana na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa uchukuaji,utunzaji,ufungashaji na usafirishaji wa sampuli hizo za chunguzi.

“lengo la mafunzo haya ni kukumbushana na kuepeana uelewa kuhusu taratibu uchukuaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa jinai, tiba na vinasaba ambapo madaktari wanafunzi kama wadau muhimu inabidi kuwakumbusha ili wanapokwenda kwenye maeneo yao ya kazi na kukutana na uhitaji kwa kuchukua sampuli za namna hiyo kutambua mambo ya msingi ya kuzingatia ili kuwezesha kupata sampuli inayokidhi vigezo kwa ajili ya uchunguzi na kutoa majibu sahihi na kwa wakati.

Hivyo, mafunzo haya yanasaidia kuwakumbusha madaktari  jukumu lao  kisheria kuhusu uchukuaji, upakiaji, utunzaji na usafirishaji wa sampuli za uchunguzi wa jinai, tiba na vinasaba ili kuweza kusaidia uchunguzi wa kimaabara kufanyika kwa mafanikio.”

Kiongozi wa wanafunzi hao, Simon Matajiri, akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa Udaktari alisema anaishukuru Serikali kuipitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo kwa sababu yameweza kuwaongezea uelewa mpana kuhusiana na masuala ya uchukuaji wa sampuli na yatawasaidia katika kazi zao na wanaahidi kwa niaba ya wanafunzi wenzake kuyazingatia yale yote waliyofundishwa.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.