CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Kanda ya Mashariki imetoa mafunzo ya siku mbili kwa wasimamizi wa Kemikali zaidi ya Arobaini kutoka kampuni thelathini kwa lengo la kuwajengea uelewa wa namna ya uhifadhi na utunzaji bora wa kemikali.

Akiongea kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi,  David Elias, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wasimamizi wa kemikali kwa kuwa yatawapa uelewa wa kujua madhara ya kemikali kwa binadamu, wanyama na mazingira licha ya faida nyingi za kemikali katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.

“Sheria inamtaka kila mdau anayejishughulisha na kemikali kwa kuingiza, kusafirisha, kuuza, kusambaza na kutumia kemikali anapaswa kusajiliwa na Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye Msajili wa wadau wote wanaojihusisha na kemikali nchini, hivyo, kupitia mafunzo haya anawataka kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wadau kupata mafunzo na kueneza elimu katika maeneo yenu ya kazi ili kulinda afya za watu na mazingira” alisema.

Nao washiriki wa mafunzo kwa upande wao wameishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo wamesema yamewaongezea maarifa na uelewa juu ya uhifadhi na utunzaji wa kemikali.

Tunatamani mafunzo haya yangeongezwa muda ili yafanyike kwa siku angalau nne, maana yamekuwa na manufaa na ni mazuri sana kwetu, tunaona muda umekuwa mdogo na bado tunahitaji hii elimu alisema Cecilia Mawala.

Mafunzo haya kwa wasimamizi wa kemikali yamefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 02 mpaka 03 Novemba 2021 kaika ukumbi wa Hazina jijini Dar es Salaam.

 

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.