Zoezi la ukaguzi wa Ubora wa Mifumo ya ISO 17025:2017 limekamilika tarehe 22 Novemba, 2022 kwa kuwapitisha wataalam wengine watano wapya kuwa wahakiki na waidhinishaji wa taarifa za matokeo ya uchunguzi wa Vinasaba (Technical Signatories) katika Maabara ya Uchunguzi wa Vinasaba vya Binadamu.
Kuidhinishwa huko kwa Wataalam hao kunapelekea Maabara ya Vinasaba (DNA) kuwa na wataalam kumi na moja (11) ambao wanatambulika katika uchunguzi wa Vinasaba ngazi ya kitaifa na kimataifa.
Taarifa za matokeo ya uchunguzi wa Vinasaba vya Binadamu zinazohakikiwa na kuidhinishwa na wataalam hao, zitatambulika, kuaminika na kutumika katika Mahakama na Mamlaka zingine zilizo nje ya Tanzania, hivyo kupanua wigo wa Maabara ya Vinasaba kupokea na kuchunguza sampuli zinazotoka nje ya Tanzania na kuiongezea hadhi Mamlaka katika wigo wa kimataifa.
Zoezi la ukaguzi wa ISO 17025:2017 lilifanyika kwa siku mbili mfululizo na kusimamiwa na Bodi ya Ithibati za Maabara Ukanda wa nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara (SADCAS) ambayo Makao Makuu yake yapo nchini Afrika ya Kusini