CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA),your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law,Read More>>

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima, ameitaka Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanyia kazi changamoto za kiutendaji ambazo Mamlaka inakumbana nazo kwa lengo la kuboresha utendaji wa kazi.

Waziri Dkt. Gwajima, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya pili ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Pamoja na mafanikio makubwa ambayo Bodi iliyopita iliweza kuyapata, bado kuna changamoto ambazo kama Wajumbe wa Bodi wapya mnapaswa kuanza nazo na kuzipa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu yenu. Baadhi ya changamoto hizo ni kuangalia uwezekano wa kuongeza motisha kwa Watumishi kutokana na unyeti na ugumu wa kazi wanazofanya. Changamoto nyingine ni deni ambalo Mamlaka inadai kutoka kwa taasisi za Serikali ambalo kwa sasa linafikia kiasi cha Shilingi Bilioni 14.4.’’

Hivyo, mimi binafsi na Wizara, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali tuna matumaini makubwa kutoka kwenu ya kututoa hapa tulipo na kutupeleka mbele zaidi kiutendaji. Ni imani yangu kwenu kuwa kwa kipindi mtakachokuwa Wajumbe wa Bodi, mtaweza kukidhi  kiu na matarajio hayo“

Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima aliendelea kusisitiza wajumbe watambue wameteuliwa kwa kuzingatia sifa zao, uzalendo na weledi hivyo kutambua kuwa jukumu walilopewa ni kubwa kulingana na hadhi ya taasisi na kuwataka kwenda kufanyia kazi suala la gharama za uchunguzi wa dawa asili.

‘‘Kazi yenu inahitaji uzalendo mkubwa sana maana ina majaribu mengi kulingana na chombo hiki. Mmeaminiwa, mmechunguzwa na mmepitishwa kwenye mifumo na kuonekana mnafaa kuongoza taasisi hii.  Mkalifanyie kazi eneo la uchunguzi wa tiba asili. Mna kazi ya kuandaa gharama na tozo za uchunguzi wa dawa za tiba asili ili kuweza kuona namna ya kusaidia eneo hili. Kwa uwekezaji uliofanywa na Serikali ndani ya taasisi hii naamini ni taasisi kubwa sana katika ukanda wa Afrika Mashariki, kwa hiyo tunapoelekea katika mfumo wa Bima ya Afya kwa wote mnahitajika kushirikiana kwa kutoka kwenda kuona taasisi nyingine kama hii katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuona namna ya kusaidiana kwa kufanyakazi pamoja huku mkiangalia kipi hawana nasi tunacho na kuweza kushrikiana katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.

Natumaini Bodi mpya itaipeleka mbele taasisi hii kiutendaji na kukidhi kiu na matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wadau na wananchi wote kwa ujumla kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na kanuni mbalimbali na kuinua kiwango cha utendaji cha Mamlaka“ alimaliza.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiongea kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, alisema Majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yameainishwa kwenye kifungu cha tano cha Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria Na. 8 ya Mwaka 2016. Majukumu haya yanaweza kugawanywa katika maeneo makuu matatu. Jukumu la Kwanza ni kufanya uchunguzi wa kimaabara wa sampuli/vielelezo mbalimbali, Jukumu la Pili ni kusimamia utekelezaji wa Sheria tatu, ambazo ni Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.8 ya mwaka 2016, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Sheria Na. 3 ya mwaka 2003 na Sheria Kusimamia na Kudhibiti Matumizi ya Vinasaba vya Binadamu, Sheria Na. 8 ya mwaka 2009 na Jukumu la Tatu ni Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali, Wadau na Wananchi wa ujumla kuhusiana na masuala mbalimbali ya uchunguzi wa kimaabara.

Copyright ©2022 Government Chemist Laboratory Authority. All Rights Reserved.

Designed and Mantained by GCLA ICT Team.