Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa Wanafunzi wa Taaluma kutoka Jeshi la Polisi. Mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha Taaluma cha Polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam Machi 13, 2025. Jumla ya Maafisa 1100 wameshiriki katika mafunzo hayo.
Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Taaluma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Andrea Legembo, akizungumza na wawezeshaji kutoka Mamlaka (hawapo pichani) mara baada ya kufika katika Chuo cha Taaluma cha Polisi kilichopo Kurasini, Dar es Salaam, Machi 13, 2025.
Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (aliyesimama) akielezea majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa Wanafunzi wa Taaluma kutoka Jeshi la Polisi kwenye mafunzo yaliyofanyika Machi 13, 2025, Kurasini, Dar es Salaam.
Maafisa wa Jeshi la Polisi walioshiriki Mafunzo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu usimamizi wa sampuli za jinai na masuala ya usimamizi na udhibiti wa kemikali katika mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Taaluma cha Polisi kilichopo Kurasini, Dar es Salaam.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai Kemia, Joyce Njisya, akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi na Upokeaji wa Sampuli za Sayansi Jinai Kemia kwa Maafisa wa Polisi waliopo katika Chuo cha Taaluma cha Polisi kilichopo Kurasini, Dar es Salaam.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai, Baiolojia na Vinasaba, Fidelis Bugoye (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu taratibu za kuzingatia wakati wa uchukuaji, utunzaji na usafirishaji wa sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba
Mwenyekiti wa Wanawake GCLA, Veronica Chiligati (katikati) akiwa na watumishi wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka MOI, Theresia Tarimo (kulia) baada ya kukabidhi misaada kwa ajili ya watoto wenye uhitaji katika hospitali ya MOI tukio lililofanyika Machi 14, 2025, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Wanawake GCLA, Veronica Chiligati (kushoto) akikabidhi risiti za manunuzi za misaada mbalimbali kwa niaba ya wanawake wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili - MOI, Theresia Tarimo (kulia), wakati walipotembelea watoto wenye uhitaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili, jijini Dar es Salaam Machi 14, 2025.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Theresia Tarimo (kushoto), akipokea msaada kutoka kwa watumishi wa Mamlaka walipo wasili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili, jijini Dar es Salaam Machi 14, 2025.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda (kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Christopher Kadio (kulia) wakati alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwa ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwatembelea wadau wa Mamlaka katika Mkoa wa Mwanza Machi 10, 2025.