Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

GCLA Logo
ISO 9001:2015 Certified

Tofauti kati ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)

 

  • Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ina wajibu wa kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha ubora na usalama wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
  • Shirika la Viwango Tanzania (TBS) majukumu yake ni kusimamia na kulinda ubora wa bidhaa na chakula katika sekta ya viwanda na biashara
  • Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kisheria ndiyo Maabara Kuu ya Rufaa ya Serikali kwenye masuala yote yanayohusu uchunguzi wa kiamaabara na matokeo yake ni ya mwisho. Maabara pekee ya Serikali yenye jukumu la kufanya uchunguzi wa vielelezo vyote ikiwemo vielelezo vya vyakula na dawa pale vinapohusisha jinai au pale sampuli/vielelezo hivyo vinapohusisha maslahi ya taifa.