Chief Govt. Chemist

Prof. Samwel V. Manyele
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YASIMIKA MTAMBO MPYA WA KISASA KWA AJILI YA UCHUNGUZI

Serikali kupitia Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kununua mtambo mpya na wa kisasa wa Energy Dispersive X – Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara kutambua aina na kiasi cha madini (metals) yaliyomo kwenye sampuli inayofanyiwa uchunguzi.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alisema kuwepo kwa mtambo huo ambao umefungwa kwenye Maabara ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, inakuwa ni suluhisho kwa wadau wote wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini ambao walikuwa wanahitaji kujua usalama na ubora wa bidhaa zao.

“Mtambo huu umesimikwa tarehe 21-23 Februari, 2017 kwenye Maabara yetu ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, kuwepo kwa mtambo huu inakuwa suluhisho kwa Serikali, Wizara, Idara na Taasisi zake, Viwanda, Mashirika, wachimbaji wakubwa na wadogo wa dhahabu na madini mengine, wachimbaji wageni, wajasiliamali na wananchi ambao walikuwa wanahitaji kujua ubora na usalama wa bidhaa mbalimbali za viwandani na kilimo.”

Akizungumzia kazi zinazofanywa na mtambo huo, Profesa Manyele, alisema unaweza kutambua kiasi cha madini yaliyopo kwenye udongo, vyakula kama vile mboga mboga zinazolimwa mabondeni, maji, mafuta, sampuli za migodini hasa kuchenjua dhahabu. Pia kubaini ubora na usalama wa bidhaa kama simenti, makaa yam awe na bidhaa za chuma.

“Mtambo huu utatumika kufanya uchunguzi wa sampuli za migodini kama miamba, udongo, masalia ya mchanga unaobaki baada ya kuchenjua dhahabu, maji taka yaliyo na chemikali ya cyanide, kubaini ubora na usalama wa bidhaa za viwandani kama vile simenti, makaa ya mawe, bidhaa za chuma, mafuta ikiwemo mafuta ya kula, petrol, dizeli na vilainishi ili kupima kiwango cha madini ya “Sulphur” na “Phosphorus.”

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Manyele, aliongeza kwa kusema mbali na kazi hizo mtambo huo utasaidia Serikali katika kufanya uchunguzi wa sampuli zitakazopatikana au kuhusishwa kutumika katika makosa ya jinai.

“Pia mtambo huu utasaidia Serikali katika kufanya uchunguzi wa sampuli na vielelezo vinavyohusiana na makossa ya jinai kama vile vioo, mabaki ya unga wa risasi, wino na rangi vilivyotumika katika uhalifu.

Vile vile itawezesha Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutekeleza Sheria ya Usimamizi na udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Sura 182, hususani uchunguzi wa ubora na usalama wa kemikali mbalimbali na bidhaa zake zinazoingizwa nchini na kusafirishwa nje ya nchi.”

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.