Chief Govt. Chemist

Prof. Samwel V. Manyele
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
MTAMBO WA ED-XRF WAZINDULIWA MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Mhe. William Ntinika, amezindua mtambo mpya  na wa kisasa wa Energy Dispensive X-Ray Fluorescence (ED-XRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara katika Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, Mhe. Ntinika, aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, alisema mtambo huo utakuwa ni jibu kwa wachimbaji  na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa madini kwa sababu wataweza kupima na kutambua kiwango cha madini kilichomo kwenye mchanga kabla ya kuchimba ili kuweza kuwekeza katika sehemu ambazo zitakuwa na faida pia kubaini ubora na salama wa bidhaa.

“Nimejulishwa kuwa mtambo huu utatumika katika kufanya uchunguzi wa sampuli za migodini kama vile miamba, udongo, masalia ya mchanga unaobaki baada ya wachimbaji wadogo kuchenjua dhahabu na maji taka yaliyo na Sianidi (Cyanide tailing solutions) na “carbon” ili kuweza kutambua kiwango cha dhahabu na madini mengine ya thamani kabla ya kuwekeza katika uchimbaji na uchenjuaji huo. Mtambo huu pia utatumika kubaini ubora na usalama wa bidhaa za viwandani kama vile saruji na “clinker”,  makaa ya mawe (coal), bidhaa za chuma, bidhaa za petroli ikiwemo mafuta ya dizeli, petroli na vilainishi ili kupima kiwango cha madini ya “Sulphur” na “Phosphorus”.

Mbali ya faida za mtambo huo ambazo alizieleza, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Ntinika aliongeza kwa kusema mtambo huo umefungwa Maabara ya Kanda za juu Kusini kutokana na uhitaji wa wananchi pia kupunguza gharama za usafiri kwa wachimbaji na wafanyabiashara kutokana na unafuu wa uendeshaji wa mtambo huo ambao hautumii vitendanishi.

“Mtambo huu umesimikwa kwenye Maabara ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya ili kuhakikisha kuwa shughuli za uchunguzi wa kimaabara zinasogezwa karibu na wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kama Mbeya, Songwe, Njombe na Katavi ambako kumeonesha uhitaji mkubwa zaidi wa huduma hiyo. Pia kuwepo kwa mtambo huu katika Maabara ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya kutapunguza gharama za kusafirisha sampuli kwenda Dar es Salaam kwa uchunguzi.”

“Faida nyingine za mtambo huu ni pamoja na nafuu ya uendeshaji kwani mtambo hautumii kemikali na vitendanisha (Reagents), unatumia muda mfupi, unaweza kuchunguza sampuli 6 kwa mpigo, gharama za uchunguzi zitakuwa chini na nafuu, mtambo huchapisha matokeo kupitia kopmpyuta na taarifa hutunzwa, ni rahisi kutumia na kuelekeza watumiaji na unachukua nafasi ndogo ya maabara.”

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, akiongea wakati kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mhe. Ntinika, alisema, Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzisogeza karibu na wananchi lakini pia kuboresha utendaji wake kwa kuongeza watumishi, kukarabati na kuongeza majengo na kuongeza mitambo ya kisasa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara.

“Maabara katika Katika kutekeleza majukumu yake, Wakala umekuwa ukifanya jitihada mbalimbali zikiwemo kupanua sehemu za kufanyia kazi kwa kukarabati na kuongeza majengo, kuongeza vifaa na mitambo ya kufanyia uchunguzi pia kuongeza idadi ya watumishi na ujuzi au utaalamu zaidi kulingana na teknolojia ya kisasa pamoja na kuanzishwa kwa maabara za kanda ili kusogeza huduma karibu na jamii.”

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.