Chief Govt. Chemist

Prof. Samwel V. Manyele
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
WAKALA YAZINDUA KAMATI MPYA YA UKAGUZI WA NDANI

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa David Ngassapa, amezindua kamati mpya ya ukaguzi wa ndani ya Wakala tarehe 19/04/2017 kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Makao Makuu ya Wakala, Dar es Salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa Ngassapa, alisema anawapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kuteuliwa kwa kuwa ndio kamati inayopitia utekelezwaji wa sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazosimamiwa na kutekelezwa na Wakala pia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 pamoja na kanuni zake.

“Kamati hii ni mifano michache ya utekelezaji wa sheria unaozingatia
uwazi na ushirikishaji wa Serikali, ambao unatupa nafasi ya kubeba ushauri, mawazo, maoni juu ya ripoti mbalimbali zinazowasilishwa kwenu na wakaguzi wa ndani wa Wakala. Kamati hii inayo majukumu muhimu yatakayoainishwa vyema na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi anayesimamia “Quality Assurance” kutoka ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali.

Uzinduzi wa kamati ya Ukaguzi wa Ndani ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya Sheria mama “Public Finance Act’ 2001. Lengo ikiwa ni kumshauri Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusiana na utekezaji bora wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia utekezaji wa taratibu za fedha, manunuzi, utumishi, usimamizi na utekelezaji wa sheria na kanuni mbalimbali zinazosimamiwa na Wakala.”

Akizungumzia majukumu ya kamati, Profesa Ngassapa, amewaasa kusimamia weledi na kuhakikisha wanatelekeza majukumu yao kwa ufanisi huku wakizingatia uwajibikaji, kutambua nafasi ya kila mjumbe, kuepuka mgongano wa kimaslahi na kuzingatia taratibu za uendeshaji wa vikao.

“Mtambue mipaka ya majukumu yenu kama kumshauri Mkemia Mkuu wa Serikali, ambaye siye mjumbe wa Kamati, mmeteuliwa kama sehemu ya utekelezaji wa sheria, mjue wajibu wenu, "obligations", Kusiwe na nia ya kupenyeza "interest" za taasisi zenu ambazo zitafifisha kazi ya kamati yenu, Kusiwe wajumbe wa kuhodhi vikao, wote wapewe nafasi sawa na kuzingatia taratibu za kuendesha vikao kama zilivyoainishwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi.”

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, kwa upande wake akitoa shukrani zake alisema anashukuru kamati hii imezinduliwa katika wakati ambao Wakala imepata hati safi kutokana na kufanya vizuri katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2015/2016 hivyo anaamini kuzinduliwa kwa kamati hiyo itasaidia kuendeleza mafanikio hayo.

“Nashukuru kamati hii imezinduliwa wakati muafaka kwa sababu ukaguzi uliopita tumefanikiwa kupata hati safi  hivyo tunaamini kamati hii itaendelea kutupa hati safi ili kuendeleza kuimarisha sifa na muonekano wa taasisi yetu mbele ya jamii.”

Naye mwenyekiti wa kamati ambaye pia ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bi. Mbonimpaye Mpango, alisema wanashukuru kwa kuaminiwa na kupewa jukumu la kuongoza kamati hiyo huku akiahidi kufanyakazi hiyo kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kuzingatia miongozo iliyopo na kuisaidia Wakala kwenda mbele zaidi.

“Nashukuru waliofanya kazi hii ya kututeua kufanya kazi ndani ya Wakala, kwa niaba ya wajumbe naahidi tutafanya kazi kwa kuzingatia miongozo na Mkaguzi wa Ndani atafaidika na uwepo wetu kwa sababu tutamuongoza vizuri. Ili Taasisi iende mbele kamati ya Ukaguzi inatakiwa kusimamia majukumu yake na ushauri unaotolewa kwenye Menejimenti na menejimenti kutekeleza kwa ufanisi ili kuleta tija kwenye Taasisi,” alimaliza. 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.