Chief Govt. Chemist

Prof. Samwel V. Manyele
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
MKEMIA ATOA UFAFANUZI KUHUSU UHALALI WA KAMPUNI YA TEKNO NET SCIENTIFIC

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele ametoa ufafanuzi wa suala linalohusiana na uhalali wa usajili wa kampuni ya Techno Net Scientific Ltd inayojihusisha na uingizaji  na uuzaji wa kemikali nchini  zikiwemo kemikali bashirifu kwenye Viwanda, Maabara za shule, Vyuo Vikuu, Taasisi za Uchunguzi na Utafiti na hospitalini nchini.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Profesa Manyele, amesema kampuni hiyo ilisajiliwa mwaka 2014 na kupewa kibali cha muda wa miaka miwili ambacho kimeisha mwaka 2016 na ilikuwa imewasilisha maombi yake ya kupatiwa kibali kipya lakini iliendelea kufanya biashara ya kemikali kabla ya kibali kutoka ambapo ni kinyume cha sheria.

“Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilitoa usajili wa muda wa miaka miwili (2) kwa kampuni ya Techno Net Scientific Ltd na kutoa namba ya usajili 9331-94–0046 tarehe 30 Aprili, 2014; usajili ambao muda wake wa usajili ulikwisha tarehe 30 Aprili 2016.  Baada ya muda wa usajili kuisha kampuni hii iliwasilisha maombi ya kuhuisha usajili wake ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali ilipaswa kusitisha shughuli zake hadi pale cheti cha usajili kitakapopatikana.

Hata hivyo, kampuni hiyo iliendelea na shughuli za kemikali pamoja na kuwa muda wa cheti cha usajili umekwisha. Aidha, kuna taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ikiingiza kemikali nchini kwa kutumia njia za udanganyifu ikiwa ni pamoja na kutumia vibali vya bandia, Kufuatana na taarifa mbalimbali za kufanya kazi kinyume cha Sheria, mamlaka za usimamizi ikiwa ni pamoja na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya na Mamlaka ya Chakula na Dawa zilifanya ukaguzi wa pamoja. Taarifa ya pamoja ya ukaguzi huo, imepelekea vyombo vya dola kuanzisha uchunguzi kuhusiana na shughuli za kampuni hiyo.”

Akizungumzia uwepo usajili wa kwanza wa kampuni hiyo pamoja suala la elimu ya watendaji wake na maghala yake kuwepo karibu na makazi ya watu, Profesa Manyele, alisema inawezekana wakati wanasajili walitumia wataaluma wenye taaluma zilizohitajika kisheria hivyo yawezekana waliondoka baadae kwa sababu wakaguzi lazima walikagua na vyeti vyao wakati walipoenda kukagua kwa ajili ya kupata cheti cha kwanza cha usajili.

“Wakaguzi wanapofanya ukaguzi lazima waangalie na vyeti vya watendaji waliopo na pia maghala yamewekwa sehemu gani, anaweza katika siku ya kwanza wakati anaomba kibali alionyesha vyeti vya watendaji ambao baadae waliondolewa, sasa wale ambao tuliwakuta kwa sasa wasingeweza kupata kibali kama wangeonyeshwa siku ya kwanza.

Naomba niliachie suala hili vyombo vingine vifanye uchunguzi ili kujua tutapata uhakika nini kimetokea, kwa sababu nyingine ni kwamba kuna maghala mengine hii kampuni ilikuwa haijaainisha na yalikuwa kwenye vificho tumeyakuta Moshi na Bagamoyo ambayo yalikuwa hayajatajwa kwamba yanahifadhi kemikali yeyote.”

Akimalizia, Mkemia Mkuu wa Serikali aliwaomba wadau wote nchini hasa wanaojihusisha na biashara za kemikali na wananchi wote kwa ujumla kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa makampuni na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu na wanaovunja Matakwa ya Sheria katika uingizaji, usafirishaji, uhifadhi na utumiaji wa kemikali ikiwemo kemikali bashirifu nchini.

 

 

 

 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.