Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
WAKALA YASHINDA NAFASI YA TATU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE KUTOKANA NA UBORA WA HUDUMA ZITOLEWAZO KWA SERIKALI NA UMMA

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeshinda nafasi ya tatu kwenye kipengele cha Wizara na Sekta za Serikali zinazotoa huduma kwa Jamii katika maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Akiongea baada ya kukabidhiwa zawadi ya kikombe na Mgeni Rasmi wa tukio hilo la kufunga rasmi maonesho ya Nane Nane Kitaifa Mkoani Lindi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba vya Binadamu, Bw. David Elias, alisema kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali, anatoa pongezi kwa watumishi wote waliofanikisha kupatikana kwa ushindi huo kutokana na namna walivyoweza kueleza kwa ufanisi shughuli zinazofanywa na Wakala na wananchi na wananchi kupata ufahamu zaidi ikiwemo kuuliza maswali.

“Ni jambo la kujivunia kwa kweli na napenda kuwapongeza wote kwa namna mlivyoweza kuwafahamisha watu shughuli za Wakala kwa kina na wananchi kuelewa na wengine kuuliza maswali yaliyokuwa yanawasumbua muda mrefu kuhusiana na Taasisi yetu. Hii inatupa changamoto ya kuongeza juhudi zaidi katika shughuli zetu ikiwemo kuwafikia zaidi wananchi ambao wanahitaji huduma zetu katika maisha yao ya kila siku.

Huu ni ushindi wa mwaka wa pili mfululizo kwa Maonesho ya Nane Nane na wa pili ndani ya miezi miwili, maana tuliweza pia kushinda tena kwa mwaka wa pili kwa kushika nafasi ya pili kwenye Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Saba Saba na sasa tumefanikiwa kushinda tena na Nane Nane.

Katika Maonesho hayo ya Nane Nane Wakala iliweza kujitangaza kwa kuonana na wananchi na kuwaeleza kwa kina shughuli zinazofanywa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoka kwa watumishi wenye weledi katika masuala yanayohusu Kemikali na Huduma za Vinasaba vya Binadamu, Sayansi Jinai na Matukio ya Sumu. Pia Banda la Wakala lilifanikiwa kutoa huduma ya kupima utumiaji wa dawa za kulevya kwa hiari kwa watu wote ambao walipenda kufanya hivyo na vijana walijitokeza katika zoezi hilo.

Katika kipengele hicho ambacho kilijumuisha Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa huduma kwa Jamii Mshindi wa Kwanza ilikuwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na mshindi wa pili ilikuwa ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Uraia (NIDA) na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kushinda nafasi ya tatu na kukabidhiwa zawadi ya kikombe na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.