Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
WAAGIZAJI WA KEMIKALI WATAKIWA KUFUATA SHERIA YA KEMIKALI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele amewataka wadau na wafanyabiashara wa kemikali nchini kufuata Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa kemikali Nchini wanapotaka kuagiza na kuingiza kemikali nchini ili kupunguza matatizo ya kuzuiliwa kwa mizigo yao bandarini kwa muda au kutakiwa kurudisha walikoitoa.

Mkemia Mkuu wa Serikali amesema hayo leo kwenye Ofisi za Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na taratibu za uingizaji wa kemikali nchini, ambapo amesema wafanyabiashara wengine wanaagiza mizigo ya kemikali wakiwa hawajasajiliwa wala hawajapata kibali na kuanza mchakato wa kufuatilia vibali baada ya mzigo kufika na kusababisha usumbufu kwao na kwa wakaguzi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Sheria inamtaka kila anayeingiza kemikali nchini lazima awe amesajiliwa na amepatiwa hati ya usajili kabla ya kuanza kujishughulisha na biashara ya kemikali. Kwa hiyo, mfanyabiashara anatakiwa kuomba kibali ili kupata idhini kabla ya kuingiza mzigo wa kemikali nchini. Ila tatizo ni wafanyabiashara wengi wamekuwa na utaratibu wa kuagiza kwanza mizigo na inapowasilis au kukaribia kufika ndipo wanaanza kuomba vibali na wengine usajili ambapo ni kinyume na sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa kemikali.

Mkemia Mkuu wa Serikali alisisitiza, kuagiza kemikali kabla ya kusajiliwa au kuwa na kibali ni kinyume ya sheria na unaweza kusababisha athari kama kuzuiliwa mzigo endapo ataingiza kemikali zisizoruhusiwa na kutakiwa kurudisha alikoutoa, mrundikano wa mizigo bandarini ikisubiri vibali, kufanyakazi kwa shinikizo hali ambayo inayoweza kupelekea makosa katika uhakiki wa nyaraka za utoaji wa mizigo na usafirishaji.”

Kutoka na hali hiyo ya kukiukwa kwa taratibu za kisheria na baadhi ya wadau wa kemikali, Mkemia Mkuu wa Serikali amesema Ofisi yake imeamua kuanzia sasa kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na changamoto hizo ikiwemo kuwaelimisha wadau kuhusiana na matakwa ya sheria, kuwachukulia hatua wanaokiuka matakwa ya sheria, kuboresha utendaji wa kazi za ukaguzi, kutoa mafunzo kwa wadau kuanzia sasa na wafanyabiashara wote wa kemikali kutojihusisha na biashara hiyo kama hajasajiliwa kwa maana hakuna mzigo utakaoruhusiwa kuingia nchini wala kutoka bandarini kwa mfanyabiashara ambaye hajasajiliwa.

“Kuanzia leo tarehe 17 Agosti 2017 hakuna atakayeruhusiwa kujishughulisha au kuingiza mizigo ya kemikali kama hana hati ya usajili au kuwa na kibali cha kuingiza kemikali. Maombi yote ya vibali lazima yaambatanishwe na hati ya usajili,mzigo utakaokuja uwe na “label” ya lugha ya Kiswahili au kiingereza tu ili kuingizwa nchini na vinginevyo utarudishwa nchi ulikotoka, kampuni ambazo hazina usajili kutoka kwa Msajili wa Kemikali hazitaruhusiwa kuingiza kemikali na kulazimika kutumia kampuni ambazo zimesajiliwa na hakuna mdau atakayeruhusiwa kushiriki tenda za ununuzi wa kemikali bila kuwa na usajili.”  

 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.