Chief Govt. Chemist

Dr.Fidelice M.S.Mafumiko
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
MKEMIA MKUU AWAASA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII MASOMO YA SAYANSI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, amewaasa wanafunzi wasome masomo ya Sayansi kwa bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao na kuja kulisaidia taifa katika tafiti za kisayansi na kufanya kazi za uchunguzi wa kimaabara zinazofanywa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Profesa Manyele ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari ya Kibaha walipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kujifunza namna shughuli za uchunguzi wa kimaabara zinavyoendeshwa.

“Napenda kuwakaribisha sana ili muweze kujifunza uchunguzi wa kisayansi unavyofanyika ndani ya Taasisi hii ya Serikali.  Lengo, mtambue umuhimu wa masomo ya Sayansi mnayosoma yanavyotumika katika shughuli za Serikali na taifa lote nje ya darasa, ili msome kwa bidii zaidi na kutambua faida yake ya baadae kwa Taifa letu na kwako mwenyewe. Pia kuongeza juhudi ili kuja kufanyakazi katika Maabara ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mtakapomaliza masomo ya elimu ya juu.”

Mkemia Mkuu wa Serikali, aliwafahamisha wanafunzi hao pia majukumu makubwa yanayotekelezwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kama kusimamia Sheria mbili pamoja na utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Tanzania kama Nchi imeridhia na Taasisi hii kuwa moja ya watekelezaji, mfano ukiwa mkataba wa Rotterdam.

“Majukumu makubwa ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni kuendesha Maabara ya Serikali kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara wa vielelezo vya kijinai, sumu, dawa za kulevya na mazingira kwa kutumia sayansi. Pia kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali, Sheria ya Teknolojia ya Vinasaba vya Binadamu, kusimamia utekelezaji wa mikataba ya kimataifa inayohusiana na masuala ya kemikali kama ya Rotterdam, Basel na Stockholm.

Vile vile kuishauri Serikali kwa masuala yote ya kemikali pia kushiriki kufanya uchunguzi wa kimaabara inapotokea majanga, mauaji ya vikongwe, watu wenye ulemavu wa Ngozi, hoja za kijamii kama kufanya vipimo vya Vinasaba (DNA) kwa wananchi ili kutatua utata kwenye masuala kama ya urithi, ubakaji, uhalali wa baba kwa mtoto, n.k.”

Akiongea baada ya kukamilisha ziara hiyo Mwalimu, Nestory Shayo, aliyeambatana na wanafunzi hao, alisema anashukuru kwa elimu waliyoipata kwa kutembelea maabara na kuweza kuona namna uchunguzi unavyofanyika mpaka hatua ya kutoa matokeo.

“Kwa kweli tunashukuru sana kwa elimu tuliyoipata maana itasaidia hata sisi waalimu wa sayansi kuweza kuelezea kitu kwa uhalisia namna inavyokuwa. Lengo letu ilikuwa kuja kutembelea maabara ya uchunguzi wa Vinasaba vya Binadamu (DNA) lakini tumeweza kupita kwenye maabara zenu nyingine pia na kupata elimu ya kutosha, tunawashukuru sana kwa kukubali ombi letu pia kutupa elimu hii.” Alisema.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.