Chief Govt. Chemist

Dr.Fidelice M.S.Mafumiko
Chief Government Chemist (CGC)

We have become the Leading provider, Laboratory services in East Africa

Facebook   Twitter Google+
  
MKEMIA MKUU AFUNGUA MAFUNZO YA UKAGUZI KWA WATUMISHI WAPYA

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, amefungua mafunzo ya ukaguzi kwa watumishi wapya wa kada ya Wakemia na Wateknolojia thelathini wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali walioajiriwa hivi karibuni.

Akiongea katika ufunguzi huo Mkemia Mkuu wa Serikali, amewaasa watumishi hao kusikiliza kwa makini mafunzo hayo na kuyashika yale yote watakayopaswa kutekeleza, kama Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani namba 3 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2015 zilivyoainisha majukumu ya wakaguzi.

“Nawasihi msikilize kwa makini mafunzo haya ili utakapoanza kwenda kwenye ukaguzi uende kutekeleza matakwa ya Sheria na kanuni zake na sio kwa hiari yako. Kuna vifungu vya sheria  ambavyo vinakuhusu kama mkaguzi na utatakiwa kuwajibika pale utakapoenda kinyume chake. Sheria inaainisha wajibu na majukumu ya mkaguzi na pia mkaguliwa, hivyo mnapaswa kuwa makini na kuelewa majukumu na wajibu wenu.

Mkemia Mkuu wa Serikali aliainisha kuwa sheria inaagiza kukagua kiwanda, ghala na masuala yote yanayohusiana na uingizaji, utumiaji, usafirishaji na uhifadhi wa kemikali na sio mtu, hivyo wakaguzi wanatakiwa kuzijua taratibu na kuzisimamia.”

Profesa Manyele, aliongeza kwa kusema mbali ya Sheria ya Usimamizi na udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, pia watafundishwa sheria za kimataifa za masuala ya usimamizi wa kemikali na baada ya hapo wataenda kwenye mafunzo kwa vitendo kwa miezi miwili, kabla ya kurudi kufanya kazi za uchunguzi wa maabara kama jukumu kuu la Taasisi.

“Nimefahamishwa pia kuwa mtafundishwa Sheria za kimataifa za usimamizi wa kemikali, za Mikataba ya Kimataifa kama vile Basel, Rotterdam, Stockholm na Minamata. Baada ya mafunzo haya mtaenda na wakaguzi wazoefu kwenye ukaguzi ili mkajifunze kwa vitendo mtakachokuwa mmefundishwa, kwa muda wa miezi miwili.

Baada ya miezi hiyo miwili mtarudi maabara kufanya kazi za kiuchunguzi ambazo ndilo jukumu kuu la Mamlaka, na ndiyo taaluma ambayo mmesomea na kuajiriwa nayo. Maabara mtakutana na watumishi wazoefu na makini ambao watawafundisha namna tunavyofanya uchunguzi kama maabara ya Rufaa ya Serikali.”

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa kemikali, Bi. Josephine Kalima, akiongea kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali kufungua mafunzo hayo aliwakaribisha na aliwasihi watumishi hao kusikiliza kwa makini mafunzo ili kuweza kutimiza majukumu yao kwa ukamilifu watakapoanza utekelezaji wa Sheria ya kemikali, Sura ya 182.

Aidha Meneja wa Maabara ya Mazingira, Bw. Emanuel Gwae, akiongea baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo alimshukuru Mkemia  Mkuu wa Serikali kwa hotuba nzuri na kuahidi kwa niaba ya wawezeshaji wote kuwafundisha mambo yote ya msingi watumishi hao wapya.

“Napenda kukushukuru Mkemia Mkuu wa Serikali kwa hotuba nzuri yenye weledi ya ufunguzi wa mafunzo haya. Tunakuahidi kuwa tutajitahidi kwa kadri tunavyoweza kuhakikisha tunawafundisha mambo yote ya msingi na muhimu kuhusiana na ukaguzi, na kuwa yatakapokamilika watakuwa wameiva vya kutosha kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yao.”  

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.