Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAFUNZO KWA WASAFIRISHAJI NA WATUMIAJI WA KEMIKALI NCHINI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni msimamizi wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Na. 3 ya Mwaka 2003.

Kwa mujibu wa Sheria hii, kwa yoyote yule, kabla ya kujihusisha na shughuli za kemikali ikiwamo,kuagiza, kuhifadhi, kusafirisha, au kuuza, anatakiwa kusajiliwa na kuomba vibali kwa Msajili wa Kemikali Nchini, ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali. Sheria pia inawataka wasimamizi wa shughuli hizo zinazohusisha kemikali na madereva wanaosafirisha kemikali hizo, kupata mafunzo maalumu yanayohusiana na usalama wa kemikali.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                      

Wadau wetu wote mnataarifiwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali ameandaa mafunzo maalumu kwa Wasimamizi wa shughuli zinazohusisha kemikali kwenye maeneo yote kama vile wahifadhi wa kemikali (ICDs), wanaoshughulika na kemikali za Viwandani na Majumbani na madereva wanaoendesha magari yanayobeba kemikali. Mafunzo haya yataendeshwa Dar es Salaam kwa ratiba ifuatayo:

TAREHE

KUNDI HUSIKA

15-16/05/2018

Wasimamizi wa shughuli zinazohusisha kemikali

17-18/05/2018

Madereva wanaosafirisha kemikali

NB: Mafunzo haya ni kwa ajili ya wale ambao hawajapata mafunzo haya, ili kuondokana na usumbufu endapo wakaguzi wa kemikali (Chemical Inspectors) na vyombo vingine vya dola vinapo simamia utekelezaji wa sheria ya kemikali.

Tafadhali wasiliana na ofisi yetu ya Kanda ya Mashariki ili kufahamu taratibu za ushiriki kwa anwani ifuatayo:

 

MENEJA, KANDA YA MASHARIKI,

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali,

Barabara ya Barack Obama,

S.L.P. 164, Dar es Salaam,

Simu ya mezani: 022 2113383/4,

Simu ya mkononi: 0677003984/0677050813/0677050818 na 0677023431,

Email: Eastern Zone – gcla.east@gcla.go.tz

Website: www.gcla.go.tz      

 

IMETOLEWA NA:

Dkt. FIDELICE M.S. MAFUMIKO

MKEMIA MKUU WA SERIKALI

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.