Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
NAIBU WAZIRI: SERIKALI INATAMBUA MAJUKUMU YA MAMLAKA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,                        Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amesema Wizara inatambua umuhimu na unyeti wa kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa Serikali na jamii ya Watanzania.

Naibu Waziri ameyasema hayo alipokuwa anazindua Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka katika hafla fupi iliyofanyika tarehe 2 Mei, 2018, katika Ofisi za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

“Naomba mtambue kuwa, Wizara inatambua umuhimu na unyeti wa kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kulinda Afya na usalama wa watu na mazingira; mchango wake katika kutekeleza Sera ya Wizara unadhihirika kutokana na uwajibikaji katika utekelezaji wa shughuli za kisheria na uchunguzi wa kimaabara kwa kutoa matokeo yanayosaidia Mamlaka nyingine za kisheria kuweza kutoa maamuzi yenye haki na hivyo kuleta utengamano katika jamii.

Hivyo, ni matumaini yangu kuwa Bodi ninayoizindua leo itaisaidia Taasisi hii katika kutimiza wajibu wake ndani na nje ya Serikali, kuendeleza mahusiano mema na Taasisi zinazohusiana na utekelezaji wa majukumu ya siku kwa siku ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.“

Vile vile Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Ndugulile amesisitiza kutoa elimu kwa umma ili jamii iweze kufahamu majukumu ya Mamlaka na taratibu za kufuata pale wanapohitaji kupata huduma zinazotolewa na Mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

„Tutoe elimu kwa jamii na umma ili kila mtu atambue kwa mfano, nini maana ya Vinasaba (DNA), ni utaratibu gani unapaswa kufuatwa ili kupima DNA na tafsiri ya hivyo vipimo maana yake ni nini. Tujitahidi kutoa majibu ya vipimo kwa wakati ili kusaidia mahakama kutoa maamuzi na kutenda haki.“

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiongea kabla ya Mgeni Rasmi, alisema pamoja na ufanisi wa Mamlaka katika utekelezaji wa majukumu yake kuna changamoto kadhaa ambazo zinapaswa kupatiwa ufumbuzi ili kuimarisha uwezo wa Mamlaka.

„Pamoja na ufanisi katika utekelezaji wa mjukumu yetu kuna baadhi ya changamoto ambazo zinapaswa  kupatiwa ufumbuzi ili kuimarisha uwezo wetu, nazo ni upungufu wa watumishi ambapo kwa sasa Mamlaka ina watumishi 228, idadi hiyo inafanya kuwe na upungufu wa watumishi 172 kati ya watumishi 400 wanaohitajika ili kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.

Vile vile, baadhi ya mitambo kuwa na umri mkubwa na pale inapoharibika inakuwa siyo rahisi kutengeneza. Tunaishukuru Serikali kupitia Wizara yako kwa kututengea bajeti ya kununua mitambo mwaka huu wa fedha, tunaiomba Wizara yako kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo ili ununuzi wa mitambo uweze kufanyika na kuimarisha uwezo wa Mamlaka.“

Akitoa shukrani baada ya uzinduzi wa Bodi, Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka, Profesa Esther Helen Jason, alisema anamshukuru Naibu Waziri kwa kuitikia wito na kuja kufanya uzinduzi wa Bodi ili kuiwezesha kuanza utekelezaji wa majukumu yake na baadhi ya majukumu ya Mamlaka yanayohitaji idhini ya Bodi yalikuwa yamekwama kutokana na kutokukamilika kwa tukio hili la uzinduzi wa Bodi ambayo kwa mujibu wa Sheria inayounda Mamlaka, utekelezaji wa majukumu ya yake uko chini ya Bodi Tendaji.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.