Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MMS: TUTAMBUE MAJUKUMU YA TAASISI NI YETU WOTE

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewaasa watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufanyakazi kama timu na kutambua majukumu ya Mamlaka ni yetu wote na kila mmoja kuchukulia jukumu la mtumishi mwingine ni lake pia.

Dkt. Mafumiko, ameongea hayo wakati anazungumza na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini alipokuwa ametembelea kwa ajili ya kujitambulisha na kuangalia ukaguzi unavyofanyika kwenye mipaka na utekelezaji wa Sheria za Mamlaka katika kanda hiyo.

“Napenda mtambue taasisi yetu ni nyeti na imepewa majukumu makubwa, hivyo tunapaswa kutekeleza majukumu yetu kwa weledi, uaminifu na kujali kila tunachofanya. Kila mmoja wetu atumie weledi katika utendaji wa kila siku na hilo litakufanya uwe huru na amani. Tupitie Sheria na kanuni zake na kuzielewa ili kuzisimamia katika utekelezaji wa majukumu yetu.”

Vile vile Mkemia Mkuu wa Serikali, amezungumzia kufanyakazi kwa bidii na linapokuja suala la kuzungumza kuhusiana na Mamlaka basi wazungumze ambao wanapaswa kufanya hivyo.

“Tukumbuke kazi zetu tunazungumza kidogo na kutenda sana na kila kitu kinawazungumzaji wake ambapo kwa Kanda ni Meneja wa Kanda ambaye anazungumza na kutenda kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Tufanye kazi kama timu na kila mmoja achukulie jukumu la mwingine ni lake pia, kwa sababu hatutambuliki kwa majina wala elimu ila tunafahamika kama watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Tutambue majukumu yetu yanagusa wananchi na Serikali moja kwa moja hivyo ushauri wetu unatoa maamuzi ya moja kwa moja kwa jamii na Serikali. Nawapongeza Kanda ya kaskazini kwa kuvuka lengo ambalo mlijiwekea kwa mwaka huu, maana tunapimwa kwa kuwekeza zaidi kwenye malengo yetu makuu kama taasisi.”

Akiongea kabla ya kumkaribisha Mkemia Mkuu wa Serikali, kuongea na watumishi, Kaimu meneja wa Kanda ya kaskazini, Bi. Thereza Kahatano, alisema anashukuru kwa Mamlaka kumuongezea watumishi ambapo itasaidia

kuongeza kazi ya utekelezaji wa majukumu ya kanda ingawa bado idadi iliyopo haitoshi kutokana na majukumu waliyonayo.

“Tunashukuru kwa watumishi ambao tumepatiwa maana itasaidia kutekeleza majukumu yetu kwa kasi ingawa bado haitoshelezi. Naamini ndani ya mwaka huu tutatekeleza na kukamilisha malengo tuliyojiwekea. Vile vile tunaomba kuanzishwa maabara ya kiuchunguzi ambayo itasaidia kwa kuanzia baadhi ya uchunguzi kufanyika hapa hapa Kanda na kutoa majibu kwa muda mfupi badala ya kusafirisha na kupeleka Dar es Salaam. alimaliza.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.