Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAMLAKA YAIBUKA MSHINDI WA PILI KWENYE MAONESHO YA SABA SABA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kuibuka mshindi ya pili katika Maonesho ya Arobaini na mbili ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Saba saba kwenye kipengele cha washiriki bora kutoka kwenye Wizara, Idara, Mamlaka na Wakala za Serikali yaliyofanyika kuanzia Juni 28 mpaka 16 Julai 2018,  kwenye Viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam.

Mamlaka imefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo vilivyokuwa vimewekwa na majaji wa zoezi hilo. Baadhi ya vigezo hivyo vilikuwa ni utoaji huduma bora na za kuridhisha kwa wateja wanaotembelea banda husika ikiwemo ufafanuzi wa shughuli zinazofanywa na Taasisi, ukarimu wa watumishi kwa wateja na wadau wanaotembelea banda, uwepo wa huduma halisi zinazotolewa na Taasisi, maandalizi ya banda na maonesho ya kazi za Mamlaka na kuweza kuoanisha kwa vitendo kauli mbiu ya maonesho na huduma za Taasisi.

Aidha, idadi na upekee wa huduma zinazotolewa na Mamlaka kwa Serikali na Wizara zake, jamii ya Watanzania katika kuboresha uchumi na utengamano na usalama ndiyo kiini hasa cha mafanikio hayo.

Akiongea baada ya kutangazwa kwa ushindi wa nafasi hiyo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, aliwapongeza washiriki na watumishi wote wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kujituma, ushirikiano na weledi katika kufanikisha ushindi huo.

“Napenda kuwapongeza kwa ushindi huu maana ni ushindi wa Taasisi nzima kutokana na kuwepo kwa mchango wa kila mmoja katika kufanikisha hili hata kama si sehemu ya watumishi walioko kwenye maonesho haya ya Saba saba. Ni fahari kwetu na faraja kwa kuendelea kushinda kwa mwaka wa tatu mfululizo na hii inaonyesha kwamba elimu tunayotoa kwa umma inasaidia jamii kufahamu majukumu yetu, hivyo ni jambo la kujivunia. Pia inaonyesha tija ya kushiriki maonesho haya kama moja ya wadau muhimu sana wa maendeleo ya viwanda.

Naamini huu ni mwanzo tu wa kuendelea kutoa elimu na huduma nzuri zaidi kupitia Mamlaka na kuwafikia zaidi wateja na wadau wetu kwa lengo la kuwafanya wafahamu zaidi shughuli na huduma zote zitolewazo na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Vile vile, ushindi huu uwe hamasa ya kutufanya tujipange vizuri zaidi katika kuwafikia wadau wetu na wananchi na kuwapatia elimu zaidi.”

Katika kipengele hicho taasisi iliyoshika nafasi ya kwanza ilikuwa ni Benki Kuu ya Tanzania na nafasi ya tatu ikishikwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.