Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MMS ASISITIZA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewasisitiza wahitimu wa taaluma ya uhandisi wa Madini na Uchenjuaji madini kusimamia matumizi salama ya kemikali ili kusaidia kuepusha uharibifu wa mazingira na afya ya binadamu.

Mkemia Mkuu wa Serikali ameyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo ya siku tatu ya Usimamizi Salama wa Kemikali kwa wahitimu wa Shahada ya Uhandisi wa Madini na Uchenjuaji Madini kutoka Chuo cha Sayansi ya Ardhi (CoES) ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

“Kemikali zina faida nyingi katika maisha yetu ya kila siku ila zinaweza kuwa na madhara makubwa endapo hazitatumika katika hali ya usalama. Natambua mmemaliza masomo yenu ya Shahada ya uhandisi wa madini na naamini taaluma yenu kazi zake nyingi mtakuwa mnatumia kemikali, hivyo mafunzo haya maalum juu ya matumizi salama ya kemikali itawasaidia sana kwenye kutekeleza majukumu yenu vile vile mtakuwa mabalozi wetu wazuri popote mtakapokuwa.

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatambua umuhimu wa matumizi salama ya kemikali ndio maana tunajitahidi kutoa mafunzo kama haya kwa wadau na elimu kwa umma ili kuwezesha kutambua umuhimu wa matumizi salama ya kemikali na vile vile matumizi mabaya ya kemikali, kwa mfano, kutumia baadhi ya kemikali kutengenezea madawa ya kulevya. Vile vile Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali imeweka adhabu kwa wadau wanaoshindwa kufuata taratibu na kanuni.”

Akiongea kabla ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Chuo cha Sayansi ya Ardhi (College of Earth Science), Profesa William Mwegoha, aliishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kati, kwa kuandaa mafunzo hayo na kuhitaji kuwe na makubaliano ya pamoja ya kutoa mafunzo hayo kwa wahitimu wanaomaliza kozi hiyo kila mwaka.

“Tunashukuru kwa mafunzo mliyowapatia wahitimu wetu kwa sababu mmewaongezea ufahamu ambao utawasaidia kuongeza uelewa katika masomo waliyosoma hapa chuoni. Nadhani kuna umuhimu wa kuwa na makubaliano ya pamoja kati ya Mamlaka na Chuo kikuu cha Dodoma ili mafunzo haya yawe yanatolewa kwa wahitimu wa ndaki ya Sayansi ya Ardhi kwa lengo la kuwapa ufahamu zaidi,” alimalizia.   

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.