Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAABARA YA KANDA YA KASKAZINI YAFANYA MNADA WA KEMIKALI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini - Arusha, imeuza kwa mnada wa hadhara kemikali aina ya “Ethyl Alcohol” iliyokuwa kwenye mapipa thelathini na sita (36) yenye ujazo wa lita mia mbili na hamsini (250) kila moja.

Mnada huo ambao uliongozwa na Bw. Ismael Ogaga, Mhakikimali wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Makao Makuu, na Bw. Timoth Mwanyingili kutoka Ofisi ya Mhakikimali wa Serikali, Mkoa wa Arusha. Mnada huo ulishuhudiwa pia na Mwanasheria wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Gilbert Ndeoruo, Kaimu Meneja Kanda ya Kaskazini,    Bi. Thereza Kahatano, Afisa Ununuzi Mwandamizi, Bw. Alfred Koya pamoja na Mhasibu wa Kanda, Bw. Cosmas Makolobelah. 

Makampuni manne (4) ya Derick Global Company Ltd kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Medics & Procurement Services Ltd, Double Diamonds Holdings Ltd, pamoja na Mega Beverage Ltd, makampuni yote yakiwa ya Mkoa wa Arusha ndio yaliyoshiriki katika mnada huo.

Katika mnada huo kemikali zilizouzwa ziligawanywa katika makundi (Lots) sita yaliyokuwa na mapipa sita kila moja. Kampuni ya Derick Global Company Ltd, ilifanikiwa kununua “Lots” tano (5) zenye jumla ya mapipa thelathini (30) kwa kiasi cha shilingi milioni kumi na tatu na laki tisa na kampuni ya Medics & Procurement Services Ltd, ilinunua “Lot” moja (1) yenye jumla ya mapipa sita kwa thamani ya shilingi milioni tatu. Wanunuzi wote walifanikiwa kulipa malipo yote na kuondoka na kemikali hizo baada ya kukamilika kwa mnada. 

Mnada huu umefanyika kufuatia wakaguzi wa kemikali wa Maabara ya Kanda ya Kaskazini, kumkamata mfanyabiashara aliyekuwa ameingiza kemikali hizo na kuzitumia nchini bila vibali vya usajili kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali mnamo mwezi Disemba 2017., Mfanyabiashara huyo alifunguliwa mashtaka,  na Mahakama kumkuta na hatia na hivyo kutoa hukumu ya kulipa faini na kunyang’anywa kemikali hizo na kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kaskazini.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.