Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAMLAKA YAUZA MAGARI KWA MNADA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Makao Makuu, imeuza kwa mnada wa hadhara magari manne ambayo yamekwisha muda wake wa matumizi kufuatana na Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali. 

Mnada huo ambao uliongozwa na Bw. Ismael Ogaga, akishirikiana na     Bw. Yese Shayo, wahakikimali wa Serikali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na Bw. Japhet Mtama kutoka Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Makao Makuu. Mnada huo ulishuhudiwa pia na Mwanasheria wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali      Bw. Gilbert Ndeoruo, Afisa Ununuzi Mwandamizi, Bw. Alfred Koya, Mhasibu Msaidizi, Bi. Agnes Ng’andu pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na washiriki wengine kutoka nje ya Mamlaka. 

Katika mnada huo magari yaliyouzwa yaligawanywa katika mafungu (Lots) manne, ambapo “lot” namba moja ilihusisha gari aina ya Nissan Patrol yenye namba za usajili STJ 9151, ambayo ilinunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni nane, “lot” namba mbili ilikuwa gari aina ya Toyota RAV 4 yenye namba STK 7689, ambayo ilinunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni tisa, “lot” namba tatu ilihusisha gari aina ya Nissan Patrol yenye namba          STJ 9671,ambayo  ilinunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni tisa na laki tano na “lot” namba nne ilihusisha gari aina ya Grand Vitara yenye namba      STJ 9150, ambayo ilinunuliwa kwa kiasi cha shilingi milioni nne baada ya  mnada kurudiwa kwa mara ya pili kutokana na mnunuzi wa kwanza ambaye alinunua kwa kiasi cha shilingi milioni tano na laki tano kuondoka kabla ya kukamilisha taratibu za manunuzi.   

Magari matatu kwa maana ya “lot” namba moja, tatu na nne ziliweza kununuliwa na Bw. Abdallah Mwichande na “lot” namba mbili iliweza kununuliwa na Bi. Frida Modest, wote kutoka Dar es Salaam. Wanunuzi wote waliweza kutimiza masharti ikiwemo kutakiwa kulipia asilimia ishirini na tano (25%) ya manunuzi papo hapo.   

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.