Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MKEMIA MKUU ASISITIZA UADILIFU KWA WATUMISHI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka watumishi wapya kuwa waadilifu na kutumia weledi katika kutekeleza majukumu yao ndani ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Dkt. Mafumiko, amesema hayo leo wakati akifungua mafunzo elekezi na upekuzi kwa watumishi wapya arobaini na sita wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

“Taasisi hii ina majukumu makubwa kwa jamii na Serikali, hivyo mtumishi unapaswa kutumia weledi katika utekelekezaji wa majukumu yako na kuwa muadilifu na muaminifu katika kuyatekeleza majukumu utakayokabidhiwa.

Unapotumia taaluma yako katika kutekeleza majukumu ya kila siku fahamu unahusika moja kwa moja na maisha ya watu wengine, jamii na nchi, kwa sababu unahusika na usimamizi wa afya za binadamu na mazingira. Unapaswa kufahamu wewe kama mtumishi  ni kioo cha taasisi na Serikali, hivyo unapotumia weledi na uadilifu katika kutimiza majukumu yako ya kiuchunguzi wa kimaabara na kutoa majibu yenye kuaminika kwa jamii na Serikali inasaidia kukupa heshima kama mtumishi pamoja na taasisi na Serikali kwa ujumla.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali, aliwafahamisha watumishi hao kuwa majukumu yote yanayosimamiwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yapo kisheria ndio maana inasimamia utekelezaji wa Sheria nne za nchi kwa sasa.

“Kila kinachotekelezwa na Mamlaka hii kipo kisheria, hivyo mtambue tunatekeleza majukumu ya Sheria nne ambazo ni Sheria inayoiunda Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.8 ya 2016, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka 2003, Sheria ya Vinasaba vya Binadamu Na. 8 ya mwaka 2009 na Sheria ya Wanataaluma wa Kemia Na. 9 ya mwaka 2016, hivyo tunapaswa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria hizo pia kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.”

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.