Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
WADAU WA KEMIKALI WAKUTANA KUJADILI UIMARISHAJI WA UDHIBITI WA KEMIKALI

Wadau wa kemikali na mazingira wamekutana Mkemia House jijini Dar es Salaam, kujadili na kutoa maoni ya maboresho ya Sheria zinazosimamia masuala ya kemikali na mazingira, ili kuzipa nguvu ya kusimamia kikamilifu udhibiti wa biashara ya kemikali ambazo zinafahamika kusababisha madhara makubwa kwa afya na mazingira, ambazo hazijaorodheshwa katika Mkataba wa Rotterdam - the Rotterdam Convention on the Prior Informed Consent Procedure for Certain Hazardous Chemicals and Pesticides in International Trade.

 Akiongea katika ufunguzi wa mkutano huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, alisema kuna kemikali na viuatilifu vinavyodhibitiwa na Mkataba wa Rotterdam, baada ya Mkutano Mkuu wa wanachama wote (Conference of Parties-COP) kuridhia ziorodheshwe. Tanzania iliridhia Mkataba huo mwaka 2004, na hivyo inautekeleza na kupata fursa ya kuzifahamu na kufanya maamuzi ya kukubali au kuzuia kemikali zilizoorodheshwa kuingia nchini.

“Utekelezaji wa Mkataba wa Rotterdam umejengwa kwenye kupashana habari katika biashara ya kimataifa kwa nchi wanachama, juu ya kemikali na viuatilifu vilivyoorodheshwa“.

Hata hivyo, kuna kemikali ambazo zimekuwa zikiwasilishwa kwa ajili ya kuorodheshwa kwenye Mkataba bila mafanikio, kutokana na baadhi ya nchi wanachama kuzuia kutokana na sababu mbali mbali, zikiwemo  za kibiashara.

Kutokana na utaratibu huo, ilikubaliwa katika mkutano hivi karibuni wa nchi za Afrika kuwa, endapo itatokea wanachama kutokubaliana na hivyo kushindwa kuorodhesha kemikali iliyowasilishwa, basi nchi zitafute njia mbadala za kulinda

watu wake na mazingira yao. Hii inatokana na ukweli kuwa kwa kuwasilishwa kikaoni, nchi zinapata taarifa kuwa kemikali husika imezuiliwa au inadhibitiwa katika nchi nyingine, kutokana na madhara kwa afya na mazingira.

 Wadau walikubaliana na kupendekeza kuwa sheria zilizopo zinaweza kutumika kudhibiti  kemikali hizo ambazo hazijaweza kuingizwa kwenye Mkataba, kwa kimarisha udhibiti kupitia mikakati mbali mbali.

Hivyo, leo tumekutana hapa kwa lengo la kupata mrejesho wa kazi ambayo Prof. Jamidu Katima, ambaye aliteuliwa na kituo cha Mikataba ya kemikali cha Kusini mwa  Afrika (Africa Institute) amefanya, pamoja na kutoa mapendekezo ya kuiboresha. Akiongea baada ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Katima alisema lengo la mkutano huo ni kupata maoni na kuboresha Sheria ili kuwezesha nchi kudhibiti kwa ubora zaidi madhara ya kemikali.

Lengo la mkutano huu ni kupata maboresho zaidi ya wadau na kama kuna Sheria nyingine wanaona zinapaswa kufanyiwa marekebisho ziweze kutambuliwa.“  Alimaliza.

Mkutano ulitoa mapendekezo kadhaa yakiwemo kuimarisha udhibiti wa kemikali katika maeneo yote, yakiwemo usajili na ukaguzi. Pia mapendekezo yalitolewa ya kutengenezwa kanuni na miongozo itakayowezesha upatikanaji wa taarifa za ziada juu ya kemikali hizo. Orodha ya Mkataba hivi sasa ina kemikali 34, baadhi zikiwa viuatilifu carbofuran na endosulfan, na kemikali za viwandani PCB na Tetraethyl lead.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.