Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAMLAKA YAIBUKA NA USHINDI KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA YA DHAHABU GEITA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeibuka mshindi wa kwanza katika maonesho ya Teknolojia Bora ya Uchimbaji wa Dhahabu yanayoendelea mkoani Geita katika kipengele cha taasisi za Serikali zinazosaidia shughuli za uchimbaji wa dhahabu na mshindi wa tatu katika kipengele cha jumla ambacho kilihusisha washindi wa kwanza wa vipengele kumi.

Akiongea baada ya kupokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason, alisema anaipongeza Menejimenti ya Mamlaka, watumishi na washiriki wote kwa ushindi.

“Napenda kuwapongeza Menejimenti, washiriki na watumishi wote wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ushindi tuliopata kwenye maonesho haya, naamini ushindi huu ni wetu wote kwa sababu Menejimenti na watumishi mmechangia kupatikana ingawa kwa njia ya ushiriki wa watumishi wachache ambao wanawakilisha wengine. Hii inaonyesha dhamira ya dhati ya taasisi yetu kuwafikia wadau wetu na kuwapatia elimu kuhusiana na huduma tunazozitoa kwa umma wa watanzania, hongereni sana na huu ni mwanzo wa kufanya vizuri zaidi kwenye maonesho na matukio mengine ambayo yanatukutanisha na wadau wetu moja kwa moja.”

Akiongea baada ya Mwenyekiti wa Bodi Tendaji, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, aliwapongeza washiriki wa maonesho kwa kuonyesha moyo wa kujituma katika kuwahudumia wadau na wakazi wa Geita waliokuwa wanafika kwenye banda la Mamlaka kwa ajili ya kupata elimu na kufahamu majukumu ya Mamlaka kwa watanzania.

“Nawapongeza washiriki wa maonesho kwa moyo wa kujituma mlioonyesha kuanzia siku ya kwanza mpaka leo. Kutoa huduma kwa watu mia nane kwa siku saba sio kitu kidogo. Naamini wachimbaji wadogo, wakubwa, wa kati, wananchi wa Geita na Kanda ya Ziwa wamepata ufahamu mkubwa kuhusiana na majukumu ya taasisi yetu na wengine naamini watakuwa mabalozi wetu huko waendako katika kueneza elimu waliyoipata kwenye masuala ya kemikali, sumu, vinasaba, mazingira na nyinginezo. Ushindi huu ni wa kujivunia kama watumishi wa Mamlaka kwa sababu inaonyesha mchango wa taasisi yetu kwa wadau wa uchimbaji wa dhahabu na wananchi wa kwa ujumla.”

Maonesho hayo ambayo yalikuwa yafungwe leo sasa yatafungwa tarehe 3 Septemba, 2018 baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongeza siku tatu zaidi.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.