Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MWENYEKITI WA BODI ASISITIZA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA UELEDI KWA WATUMISHI

Mwenyekiti wa Bodi Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason, amesisitiza uadilifu, uwajibikaji, ueledi na ubunifu kwa watumishi wakati wanapotekeleza majukumu ya kazi.

Mwenyekiti wa Bodi Tendaji amezungumza hayo leo wakati anaongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa Kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kukamilisha ziara ya kutemblea Kanda hiyo.

“Tumepewa dhamana kubwa na Serikali ambayo tunatakiwa kuilinda. Mamlaka ndio Maabara Kuu ya Serikali na Sheria inasema wazi kwamba matokeo ya uchunguzi wetu wa kimaabara ndio ya mwisho, mnaweza kuona namna taasisi yetu ilivyo ya kipekee na Serikali inaithamini na kuitazama mno. Hiyo inaonyesha wazi kwamba uadilifu unapaswa kuwa kitu cha muhimu sana kwetu kwa sababu tunabeba dhamana ya Serikali, wananchi, makundi, taasisi binafsi na za umma.

Vishawishi ni vingi mnakumbana navyo ila ni vya muda tu, simama kwenye uadilifu, tuwajibike kwa kubeba majukumu yetu kwa uhakika na kuimarisha utendaji kazi. Wajibika kwa kufanyakazi kwa kutumia taaluma yako iliyokufanya uwepo hapa leo. Tumia taaluma yako na ueledi katika utekelezaji wa majukumu ili uweze kuendelea na kutoka hatua moja kwenda nyingine, ongeza ubunifu katika kazi zako ili usilemae na kile unachojua tu bali jifunze na uliza kupitia kwa wengine ili kuongeza ufanisi katika utendaji wako.

Natambua kuna changamoto tumepitia miaka michache nyuma na baadhi ya watumishi wenzetu kuingia katika matatizo, tutambue changamoto ni sehemu ya maisha na mtu yeyote anaweza kupitia katika matatizo. Hayo yaliyotokea yasiwafanye kuwa waoga na kutotekeleza majukumu yenu bali tuchukulie kama changamoto na tuendelee na maisha wakati yaliyotokea yakiendelea kufanyiwa kazi. Kinachotakiwa ni kutekeleza majukumu yetu kwa ueledi na uadilifu mkubwa huku tukiimarisha maabara zetu ili kutoa huduma bora zaidi.”

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiongea kabla ya Mwenyekiti wa Bodi Tendaji, alianza kwa kuwapongeza watumishi wa maabara ya Kanda ya Ziwa kwa kazi kubwa wanayofanya Kanda pamoja na ukubwa wake. Vile vile aliwakumbusha watumishi jukumu kubwa ambalo Mamlaka inalitekeleza la kufanya uchunguzi wa kimaabara.

“Tunajukumu kubwa la kufanya uchunguzi wa kimaabara na kutoa majibu, kutoa ushahidi wa kitaalam Mahakamani na kusimamia Sheria tulizonazo, tunapaswa kukumbuka hayo majukumu kila tunapofanya kazi zetu. Tutambue tumepewa dhamana kubwa na Serikali kama Maabara Kuu ya Rufaa kwa Serikali ila sina uhakika kama wote tunaiona hii dhamana.

Tukitoa matokeo kwa uhakika na kuzingatia ueledi tutakuwa tumesaidia nchi na tukifanya kinyume tutakuwa tumeiangamiza nchi na taaluma zetu. Kikubwa kinachotakiwa kituongoze ni Sheria zetu na tutambue si jukumu la Mkemia Mkuu wa Serikali au Meneja bali ni la watumishi wote kuzitekeleza. Tuzitambue na kuzielewa Sheria zote tunazozisimamia na tutekeleze kwa kuzingatia dira na dhima ya Mamlaka.

Tumezunguka kwenye Kanda hii kuanzia mipakani na tumeona na kujifunza mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ikiwemo kuimarisha maabara zetu za Kanda kwa vifaa na teknolojia, shughuli za ukaguzi, kuwajengea umahiri watumishi kwa mafunzo kazini, kuimarisha vyanzo vya mapato na kuvisimamia. Tufanye kazi kama familia moja na huku tukitambua dhamana tuliyopewa na Serikali.”

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao, Meneja wa Maabara ya Kanda ya Ziwa, Bw. Bonventura Masambu, alisema mbali ya kutekeleza majukumu ya Kanda kwa mafanikio na kuongeza mapato kwa Mamlaka bado changamoto kubwa wanayokumbana nayo katika Kanda ni kuwepo kwa bajeti ndogo inayotengwa ukilinganisha na majukumu mengi na makubwa ambayo Kanda ya Ziwa inatekeleza. Pia, aliomba kuimarishwa kwa maabara ya Kanda ikiwemo kununuliwa kwa mashine ya “Cyanide Analyzer” kwa sababu ya umuhimu wake kwa Kanda ya Ziwa kutokana na kuwepo kwa machimbo mengi ya madini ya dhahabu.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.