Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
WADAU WANAOTAKA KUSIMAMIA KEMIKALI HATARISHI WATAKIWA KUJISAJILI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka wadau wanaohitaji kujihusisha na usimamizi wa kemikali hatarishi kutimiza matakwa ya Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali ya Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka 2003 kwa kujisajili.

Mkemia Mkuu wa Serikali ameyasema hayo leo wakati akifungua warsha ya siku moja iliyohusu usimamizi salama wa mizigo ya kemikali hatarishi kwa wadau wa kemikali iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Ni matumaini yangu kuwa, baada ya warsha yetu ya leo, kila mmoja atakwenda kutimiza wajibu wake kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu kama anataka kusimamia au kuhifadhi kemikali hatarishi. Ni vizuri ikaeleweka kuwa, hadi sasa ni kampuni moja tu ambayo inaendesha Bandari Kavu (ICD) ambayo imeweza kukamilisha taratibu za kuhifadhi kemikali hatarishi na kupewa kibali cha kufanya kazi hiyo na kampuni yenyewe ni PMM Estate (2001) Ltd. Nitoe rai kwa Bandari Kavu zingine ambazo zina nia ya kusajiliwa kwa ajili ya kutunza na kusimamia kemikali hatarishi zijitokeze ili ziweze kusajiliwa na kupewa kibali cha kufanya hivyo.”

Dkt. Fidelice Mafumiko, aliendelea kwa kusema kwamba wadau wanapaswa kutimiza matakwa ya msingi kisheria ambayo yanahitajika ili kuweza kupata kibali cha kuweza kuhifadhi au kusafirisha kemikali hatarishi hapa nchini huku akitoa wito kwa wadau kutumia warsha hiyo kujifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa kemikali hatarishi.

“Baadhi ya masuala ya msingi yanayohitajika katika usajili ni pamoja na kuwa na hati ya madhara kwa mazingira yaani "Environmental Impact Assessment", Mpango wa Kujikinga, mtaalamu mwenye sifa zinazotambulika kwa ajili ya usimamizi wa kemikali, mfano "Cyanide International Code Registered Expert" kama unatunza kemikali aina ya “Sodium Cyanide”, kuwa na eneo la kutosha ili uweze kutenganisha shughuli za kemikali hatarishi na shughuli za mizigo mingine, kujiandaa na kukabiliana na Majanga ya Kemikali yaani "Chemical Emergency Prevention, Preparedness and Response" pamoja na vifaa vya usalama kutegemea na aina ya kemikali hatarishi unayotaka kusimamia au kuhifadhi.

Ni wito wangu kuwa, mtaitumia warsha hii kujifunza masuala mengine mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kemikali hatarishi zinasimamiwa na kutumika salama nchini. Pia, kama nchi inayohudumia nchi nyingine kwa kusafirisha kemikali hatarishi kupitia bandari ya Dar es Salaam ni vizuri kuhakikisha kuwa tunatoa huduma bora bila kuathiri usimamizi au uhifadhi salama wa kemikali hizo.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Mhandisi Anthony Swai, alisema anaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuandaa warsha hii na kutoa elimu kwa wadau wa kemikali na ameomba isiwe mwisho bali utaratibu huo uendelee kwa maana utasaidia kuepukana na majanga yanayohusisha kemikali kwa sababu elimu inapotolewa mara kwa mara kwa wadau ndio njia ya kujikumbusha na kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa na ajali za kemikali hapa nchini.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.