Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Google+
  
MAMLAKA YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI NA WALIMU BORA ZAIDI WA MASOMO YA KEMIA NA BAIOLOJIA

Mganga Mkuu wa Serikali, profesa Mohammad Kambi, amesema Serikali imeanza jitihada za kuinua na kuhamasisha wanafunzi kupenda na kusoma masomo ya sayansi kwa lengo la kujenga msingi imara wa kuwa na wataalam wengi wa sayansi watakaosaidia Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaoongozwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Profesa Mohammad Kambi, ameyasema hayo leo wakati wa Hafla ya kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi na walimu waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo ya Kemia na Baiolojia kwenye mitihani ya Kidato cha  nne 2017 na Kidato cha sita mwaka 2018 iliyofanyika kwenye viwanja vya Jengo la Mkemia, Dar es Salaam.

“Serikali imeanza jitihada mbalimbali za kuinua na kuhamasisha watoto wetu kupenda na kusoma masomo ya sayansi lengo kuu ikiwa ni kujenga msingi imara wa kutupeleka kuwa nchi ya uchumi wa kati unaoongozwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025. Kwa kuanza Serikali imeendelea kutoka motisha wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaochukua michepuo ya sayansi kwenye vyuo vikuu vyetu vyote pamoja na kuendelea kuhamasisha ongezeko la walimu wa sayansi kwenye shule zetu zote nchini

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, taasisi ambayo majukumu yake yanajengwa na msingi mkuu kwenye taaluma ya kemia na baiolojia. Sote tunatambua majukumu yanayotekelezwa na taasisi hii ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kikemia na kibailojia wa sampuli mbalimbali, Wizara yangu kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali itaendelea na utaratibu wa kuwapatia zawadi wanafunzi bora pamoja na walimu wao waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao ya kidato cha sita na kidato cha nne pamoja na walimu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwatunuku kwa bidii na kujituma kwao katika kusoma kwa upande wa wanafunzi na kufundisha kwa upande wa walimu hali iliyowawezesha kuwaongoza wenzao.“

Mwenyekiti wa Bodi ya Tendaji ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason, amesema Mamlaka inaahidi kuendelea na utaratibu huu wa kutoa zawadi kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri zaidi ili kuendelea kutoa hamasa kwa vijana wetu kupenda masomo ya sayansi kwa sababu unatoa matumaini kwa vijana kuwa watalaamu watarajiwa wa Taasisi za kisayansi nchini.

‘‘Bodi pamoja na Menejimenti ya Mamlaka kwa niaba ya Wizara yako, na tukiwa mojawapo ya waajili wakuu wa wanataaluma wanaotokana na masomo ya kemia na baiolojia, tunakuahidi kuendelea na utaratibu huu wa kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi ili kuendelea kutoa hamasa kwa vijana wetu kupenda masomo ya sayansi. Aidha, ni imani yetu kuwa, utaratibu wa kuwapongeza waliofanya vizuri zaidi unatoa matumaini kwa vijana wetu kuwa watalaamu watarajiwa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wizara ya Afya, Taasisi nyingine za Serikali na Mashirika binafsi ambapo taaluma zinazotokana na masomo haya zitahitajika.“

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, alisema katika miaka 11 ambayo Mamlaka imekuwa ikitoa zawadi kwa wanafunzi na walimu jumla ya waliotunikiwa zawadi hizo ni wanafunzi 192 na walimu 16 ikijumuisha na wale waliopata zawadi leo. Ikikumbukwa kuwa, utaratibu wa kuongeza somo la baiolojia na kutoka zawadi kwa walimu ulianza mwaka 2015 ambapo kabla ya hapo ilikuwa somo la kemia pekee.

Aidha, amesema Shule zilizopata zawadi mara nyingi zaidi katika kipindi cha miaka 11ni Shule ya Feza Boys mara 18, St. Mary's Mazinde Juu mara  16, Mzumbe Sekondari na Marian Girls mara  14, Tabora Wavulana mara 10, Kilakala na Feza Girls mara 8. Shule zingine zilizobakia 23 zimepata zawadi kati ya mara 1 hadi 7. Hii yote inaonyesha hamasa inayotokana na utaratibu huu kwa sehemu fulani pamoja na juhudi  zingine zinazofanywa na Serikali kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi.

 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.