Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MAMLAKA YAKUTANA NA WAJASIRIAMALI WANAOJIHUSISHA NA MATUMIZI YA KEMIKALI

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekutana na wajasiriamali wadogo wanaojihusisha na matumizi ya kemikali kwa katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

 Akiongea katika ufunguzi wa warsha hiyo, Mkemia Mkuu wa Serikali,            Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema lengo la kukutana ni kuhakikisha kuwa wote wanaohusika na biashara au shughuli zinazohusisha matumizi ya kemikali wawe wanatambulika na kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani.

‘‘Lengo la warsha hii ni kuhakikisha kuwa wote wanaohusika na biashara au shughuli zinazohusisha matumizi ya kemikali wawe wamejitambulisha kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuweza kupewa cheti cha usajili kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Tumeanza kuwapa elimu na maelekezo wasambazaji wa kemikali kuacha kuwauzia wahusika wote ambao hawana cheti cha usajili kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuwezesha wajasiriamali wadogo kutimiza wajibu wenu kwa kufanya kazi kwa kufuata Sheria.

Hivyo, kikao hiki kifupi cha leo kimelenga kuwajengea uelewa juu ya matakwa  ya Sheria ya usimamizi wa Kemikali na wajibu mnaopaswa kuutimiza. Kikao hiki pia kimelenga kuwapa utaratibu wa kufuata ili kumwezesha kila mhusika kufahamu yale anayopaswa kuyatimiza kabla ya kupata cheti cha usajili wa kutumia kemikali. 

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali, alisema kati ya wajasiriamali hao kuna wanaotumia kemikali kwa ajili ya kutengenezea sabuni, mishumaa na nguo za batiki lakini wanapaswa kutambua kuna baadhi ya kemikali ambazo wanatumia ni bashirifu hivyo bila wao kujua zinaweza kutumiwa vibaya na baadhi ya watu kwa kubadilisha matumizi yake.

‘’Baadhi ya shughuli ambazo mnazifanya nyinyi wajasiriamali wadogo ambazo zinatumia kemikali ni pamoja na utengenezaji wa sabuni za miche, unga na maji; utengenezaji wa rangi; utengenezaji wa batiki, utengenezaji wa maji ya betri; utengenezaji wa mishumaa na bidhaa nyingine nyingi mnazotengeneza. Kemikali mnazotumia baadhi yake zina Madhara kwa Afya na Mazingira. Aidha, baadhi yake ni Kemikali Bashirifu ambazo zinaweza kutumika kutengeneza Dawa za Kulevya.

Pamoja na hali hiyo, ni ukweli usiopingika kuwa ni kundi ndogo sana kati yenu mnatumia kemikali hizi kihalali na kwa kufuata taratibu zinazohitajika. Hali hii inapelekea udhibiti wa kemikali hizo kwa upande wa Mamlaka za Udhibiti za Serikali kuwa siyo madhubuti kutokana na kukosekana kwa taarifa ya nani yuko wapi na anatumia kemikali ipi kufanya nini. Pia, utaratibu wa namna hii unaweza kupelekea kemikali hatarishi na bashirifu kuingia kwenye mikono ambayo siyo salama na hivyo kutumika kufanya masuala ambayo ni kinyume cha matumizi yanayoruhusiwa.“ Alimalizia.

 

 

 

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.