Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MAMLAKA YAMUELEZA WAZIRI MKUU UTOFAUTI WA MAJUKUMU NA TFDA

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imetoa ufafanuzi juu ya utofauti wa kisheria na majukumu kati yake na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Ufafanuzi huo umekuja mara baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa  kuuliza swali hilo kwa lengo la kutaka umma kufahamu tofauti iliyopo kati ya taasisi hizi mbili za Serikali kuhusiana na masuala ya uchunguzi wa vyakula na dawa mara baada ya kupita kwenye banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sheria uliofanyika leo kwenye viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma.

“Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na shughuli za uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli au vielelezo vinavyohusiana na makosa ya jinai na kusaidia vyombo vingine kutenda haki, kama vile kutoa ushahidi mahakamani kwa mashauri au kesi mbalimbali, lakini pia mnafanya uchunguzi wa vyakula na dawa, sasa nyinyi tofauti yenu na TFDA ni nini?” alisema.

Akijibu swali hilo, Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai na Vinasaba, Bi. Hadija Mwema, alisema kuna tofauti kuanzia kwenye Sheria zinazounda taasisi hizi mbili kwa kuweka utofauti wa majukumu ya msingi.

“Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kisheria ndiyo Maabara Kuu ya Rufaa ya Serikali kwenye masuala yote yanayohusu uchunguzi wa kimaabara na matokeo yake ni ya mwisho. Aidha, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kisheria ndiyo Maabara pekee ya Serikali yenye jukumu la kufanya uchunguzi wa vielelezo vyote ikiwemo vielelezo vya vyakula na dawa pale vinapohusisha jinai au pale sampuli/vielelezo hivyo vinapohusisha maslahi ya taifa.

Kwa upande mwingine, Mamlaka ya Chakula na Dawa ni Msajili wa chakula na dawa nchini kwa ajili ya kulinda usalama wa mlaji. Aidha, ili kujua usalama wa chakula au dawa husika wahusika ni lazima wasajiliwe na wakati wa usajili Mamlaka inajiridhisha kupitia uchunguzi wa kimaabara. Hata hivyo, chakula au dawa kikihusisha jinai, jukumu la uchunguzi wa kimaabara na kutoa ushahidi mahakamani huwa linahamia na kuwa la Mamlaka ya Mabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.”

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.