Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
SERIKALI KUENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI YA KEMIKALI NCHINI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kusimamia na kudhibiti matumizi ya kemikali ili kuhakikisha hazileti madhara kwa afya za wananchi na Mazingira.

Mheshimiwa Ummy Mwalimu, amesema hayo wakati akifungua Mkutano na wadau wanaojishughulisha na shughuli za kemikali ulioandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ya kemikali nchini.

“Kemikali zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara katika afya, mazingira pamoja na kuhatarisha usalama wa nchi, ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kusimamia na kudhibiti uingizaji na matumizi ya kemikali nchini ili zisilete madhara.Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za mwaka 2014 zinaonyesha vifo milioni 12.6 vilitokana na mazingira duni ya kuishi, mojawapo ya kichocheo ni athari za kemikali ambazo zimekuwa zikisababisha magonjwa na vifo.”

Mheshimiwa Waziri wa Afya aliendelea kwa kusema kemikali zimekuwa na athari kubwa kwa binadamu kwa kusababisha magonjwa zaidi ya mia moja huku akiyataja magonjwa ya moyo, saratani, ngozi, athari katika mifumo ya fahamu, upumaji pamoja na chakula kuathiri zaidi wananchi wengi.

“Tukubali kuwa kemikali zina madhara kwa wananchi lakini sasa tuwe na mazingira mazuri ya kuzidhibiti, Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri kwa wafanya biashara ya kemikali nchini.”

Kwa upande mwingine Waziri Ummy Mwalimu amezitaka Taasisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kuangalia upya tozo zinazotozwa kwa wafanyabiashara za kemikali nchini pamoja na kupunguza changamoto zisizo za lazima ili kuwawekea mazingira rafiki wafanya biashara za kemikali.

“Msiwe ni kikwazo kwa uwekezaji na biashara, kikwazo cha kushamiri na kukua kwa uwekezaji nchini, nataka muwe mawakala wa kukuza biashara na uchumi nchini ili kuvutia wawekezaji kwa kuweka mazingira rafiki kwa biashara” alimalizia Waziri Ummy.

Awali akisoma taarifa yake Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko, amesema Sheria ya Kemikali za Viwandani na Majumbani Namba. 3 ya mwaka 2003 imekuwa na mchango mkubwa katika udhibiti wa matumizi ya kemikali nchini.

“Kabla ya kutungwa kwa sheria hii, kemikali zilikuwa zikiingizwa nchini kiholela na kutumika bila ya kuwa na ufuatiliaji au udhibiti wowote ila baada ya kutungwa kwa Sheria hii imewawezesha kudhibiti usafirishaji, utumiaji pamoja uteketezaji wa taka zinazotokana na kemikali. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inasimamia kwa ukaribu matumizi ya kemikali zote zinazoingizwa nchini kuanzia zinapoingia, mahali zinapokwenda pamoja na matumizi yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Mafumiko.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) Mhandisi Anthony Swai, amesema tozo zimekuwa nyingi kiasi cha kuwaumiza wafanyabiashara huku akiiomba Serikali kuainisha mipaka ya taasisi za umma pamoja na tozo wanazostahili kulipa kwani kumekuwa na mwingiliano wa majukumu baina ya taasisi kama Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.