Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.

Facebook   Twitter Instagram
  
MKUU WA WILAYA AWATAKA WACHIMBAJI WA NAMUNGO KUZINGATIA SHERIA

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa amewataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi wa Namungo kuzingatia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali wanapokuwa wanatekeleza shughuli za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya zao na mazingira.

Mhe. Mgandilwa amezungumza hayo leo wakati anafungua mafunzo ya siku mbili ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa wachimbaji hao yanayotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini na kufanyika kwenye kijiji cha Namungo, wilayani Ruangwa.

“Nawaomba wachimbaji wa mgodi wa Namungo mtumie fursa hii ya mafunzo kujifunza Sheria zinazohusu usimamizi na udhibiti wa kemikali ili kuweza kuzingatia matumizi salama ya kemikali katika shughuli zenu za uchimbaji wa dhahabu kwa lengo la kulinda afya zenu na mazingira yanayowazunguka. Natambua uchimbaji wa dhahabu unahusisha matumizi ya kemikali na hakuna kemikali isiyo na madhara duniani. Hivyo, mafunzo haya yawasaidie kujua namna bora ya kujilinda na madhara bila kuathiri shughuli zenu za uchimbaji.

Sekta ya madini ni sekta muhimu sana katika uchumi na ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano inajitahidi kuwawekea mazingira mazuri wachimbaji ili kuhakikisha mnafaidikia na kazi yenu lakini pia kulinda afya maana athari za kemikali nyingine zinaweza kuonekana hata baada ya miaka mingi mbele na kusababisha kupoteza nguvu ya Taifa.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya aliwataka wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu wa Namungo kujisajili Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kutambulika kama wadau wanaotumia kemikali katika shughuli za uchimbaji wa madini hayo.

“Niwaombe wachimbaji wa mgodi wa Namungo kutumia fursa hii ya kupata elimu na kujisajili ili kuweza kutambulika kisheria kama wadau mnaotumia kemikali kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.  Mafunzo haya yawasaidie kujifunza namna sahihi ya matumizi ya kemikali na taratibu za kujisajili, hivyo mnapaswa kuuliza maswali pale mnapoona mnahitaji ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa wawezeshaji wa mafunzo kwa lengo la kuboresha shughuli za uchimbaji na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawajaweza kupata elimu hii kwa sasa.” Alimalizia.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,   Bw. David Elias, akiongea kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, alisema Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeamua kuwafikia wadau wake na kuwapa elimu ya matumizi ya salama ya kemikali kwa lengo la kuongeza uelewa wa masuala ya kemikali ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya na kimazingira yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali. Aliongeza kwa kusema kwamba wachimbaji wadogo wadogo wa Namungo ni sehemu ya wadau wengi ambao Mamlaka imejipanga kuwafikia na kuwapatia elimu hiyo.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji ya Gemini naye alisema anaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuamua kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimarisha shughuli zao za uchimbaji hasa kwenye matumizi ya kemikali.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kuona umuhimu wa kuja kutoa mafunzo haya kwetu wachimbaji wadogo wadogo wa Namungo kwa sababu tunaamini yatatusaidia katika kujilinda dhidi ya madhara ya kemikali kwenye kazi zetu za uchimbaji. Tunaamini mafunzo haya yatakuwa chachu kwetu ya kufuata Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali kwa lengo la kuboresha uchimbaji wetu wa dhahabu na kulinda afya na mazingira kwa ujumla.”

Mafunzo hayo yamehusisha jumla ya wachimbaji wadogo wadogo hamsini kutoka Kampuni za uchimbaji za Gemini na Majini zinazojihusisha na uchimbaji wa dhahabu kwenye mgodi wa Namungo uliopo wilayani Ruangwa katika Mkoa wa Lindi.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.