Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MKEMIA MKUU WA SERIKALI ASISITIZA WAKAGUZI KUZINGATIA WELEDI

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewasisitiza wakaguzi wa kemikali na maabara za kemia kuzingatia weledi, uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Mkemia Mkuu wa Serikali amezungumza hayo leo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Wakaguzi wa Kemikali na Maabara za Kemia kutoka Mamalaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali unaofanyika Baraza la Maaskofu, Kurasini, Dar es Salaam.

“Serikali imetupa majukumu ya kusimamia Sheria ya Mamlaka ya Maaabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria ya Vinasaba vya Binadamu na Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, hivyo tunapaswa kuzingatia weledi, uadilifu, uaminifu na upendo ili kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa ufanisi.

Tutambue Serikali yetu imejielekeza katika kujenga uchumi wa viwanda na inajitahidi kuwekeza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ikiwemo wanaojihusisha na kemikali, hivyo  tunapotekeleza majukumu yetu tunapaswa kuelewa uelekeo huo wa Serikali na kufanya maamuzi kwa wakati na haraka ili kutokwamisha wadau wetu huku  tukizingatia Sheria.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali alisema Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inawapongeza wakaguzi hao kutokana na kazi kubwa wanayofanya na inawahamasisha kuboresha zaidi huduma kwa wadau kwa kufuata Sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kama watumishi wa umma.

“Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti inatambua mchango mkubwa wa wakaguzi katika kusimamia Sheria na kuingiza maduhuli ambayo taasisi inatumia katika kuboresha huduma na kujiendesha. Tunatambua changamoto zipo na tunaendelea kuzifanyia kazi kama kuongeza watumishi na vitendea kazi. Tuna maeneo ya msingi ya kuyawekea kipaumbele hasa kwenye uwekezaji wa mitambo ya kisasa ya maabara na teknolojia ili kuwawezesha wakaguzi kutoa huduma bora na za haraka kwa wadau. Tufanye kazi kama familia ili kuweza kutekeleza majukumu yetu kwa mafanikio.” Alimaliza.

Akitoa neno la shukrani, Mkaguzi wa Kemikali, Bw. Jovitus Mukela, alimshukuru Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko kwa nasaha nzuri za ufunguzi wa Mkutano huo na kuwaomba washiriki kuzingatia yale yote yaliyozungumzwa na kushirikiana kutoa huduma nzuri na kwa kufanya hivyo watakuwa wameitendea haki Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, wao wenyewe na nchi kwa ujumla.

 

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.