Chief Govt. Chemist

Dr. Fidelice M.S. Mafumiko

CHIEF GOVERNMENT CHEMIST

Welcome to the Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), your number one centre for laboratory analysis of samples/exhibits related to Forensic Sciences in order to facilitate forensic investigations and hence assurance of justice and rule of law, samples related to agricultural and industrial produce to ascertain safety and quality, samples related to paternity or sex identification in order to address society concerns and samples related to environmental and occupational health for the protection of health and the environment.


Facebook   Twitter Instagram
  
MWENYEKITI WA BODI AWATAKA WACHIMBAJI KUZINGATIA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason amewataka wachimbaji wa madini ya dhahabu Chunya kuzingatia matumizi salama ya kemikali wanazozitumia katika shughuli zao za uchimbaji kwa lengo la kulinda afya na mazingira.
Profesa Esther Hellen Jason amesema hayo Wilayani Chunya wakati akiongea na viongozi wa wachimbaji na wamiliki wa migodi ya madini ya dhahabu.
"Ndugu zangu tuzingatie matumizi salama ya kemikali kwa lengo la kulinda mazingira, afya zetu na vizazi vyetu. Tunatambua sekta ya madini ni moja ya sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi kwa sababu dhahabu inaingiza mapato ndani ya Serikali lakini huwezi kuipata dhahabu bila kutumia, baadhi ya kemikali hivyo kuchukua tahadhari ni muhimu kwa maisha yetu na uchumi wetu maana ukiathirika na kemikali hutoweza hata kuendelea na uzalishaji tena."
Aliendelea kwa kusema anaamini kukutana na wadau na kujadiliana namna bora ya kuimarisha mahusiano ya kikazi ni njia sahihi ya kutatua changamoto na kuboresha utendaji kazi wa pande zote kama walivyofanya.
"Mfumo wa kukutana na kujadiliana naamini ni njia sahihi ya kutatua changamoto nyingi tunazokumbana nazo katika shughuli zetu za uchimbaji na  uchenjuaji wa dhahabu. Hivyo  changamoto zenu mlizowasilisha leo tunazichukua kwa uzito mkubwa  na tutayafanyia kazi ili kuboresha zaidi utendaji wetu na shughuli zenu. Kwa zile zilizo ndani ya uwezo wa Bodi ya Wakurugenzi tutazifanyia kazi kwa lengo la kurahisisha utendaji wenu na zinayohitaji maamuzi ya juu zaidi tutayawasilisha ili kupatiwa ufumbuzi maana zikitatuliwa changamoto hizi tunaamini hazitakuwa kwa faida ya Chunya tu bali kwa wachimbaji wa Tanzania nzima wanaotumia kemikali." Alimalizia
Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, akiongezea alisema Mkutano huo ni mwanzo wa ushirikiano wa Mamlaka na wachimbaji hao wenye lengo la kutatua changamoto na kuzifanya kuwa fursa za kuboresha utendaji na kuwezesha wadau hao wa Chunya na maeneo mengine ya migodi nchini huku akiamini katika mazungumzo ndio maboresho mengi yatafanikiwa, ikiwemo kutoa elimu stahiki ya matumizi salama ya kemikali.
Akiongea kwa niaba ya wachimbaji, Mwenyekiti wa Wachimbaji wa dhahabu Mkoa wa Mbeya, Leonard Manyesha, alisema anashukuru kwa mkutano huo na anaamini mazuri yaliyojadiliwa yataleta tija.
"Nimefurahishwa na mkutano huu na naamini tuliyojadili yakifanyiwa kazi yataleta tija kwenye kazi zetu za uchimbaji wa dhahabu. Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamekuaa karibu sana kwetu hasa kwenye mafunzo ya matumizi salama ya kemikali na kutatua changamoto zetu pale tunapoziwasilisha." Alimalizia.

Our Vision

To become a reputable world class analytical laboratory for executing health, social well-being and environmental interventions.

Our Mission

To provide quality and cost effective laboratory and regulatory services to the Government, Institutions, private sector and the general public for the purpose of safeguarding human health, environment and for execution of justice.